Header Ads

SHULE YADHIBITI WATOTO WA WAFUGAJI

Shule yadhibiti watoto wa wafugaji

Mkuu wsa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala
 
UONGOZI wa shule, wazazi wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Magwalisi katika Halmashauri ya Mji Mdogo wa Rujewa wilayani Mbarali, Mbeya kwa pamoja wameanzisha utaratibu wa kambi kwa wanafunzi wa madarasa ya mitihani ili kukabiliana na utoro utokanao na kuhamahama kwa wazazi ambao wengi ni wafugaji.
Wakizungumza na waandishi wa habari shuleni hapo, uongozi wa shule pamoja na vitongoji walisema walimu na wazazi walikubaliana kuchangia ili wanafunzi wa darasa la saba waishi shuleni hadi watakapofanya mitihani ya mwisho ili kudhibiti utoro.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyaluhanga B, Gorden Mgombawani alisema asilimia kubwa ya wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Magwalisi ni wafugaji na wakulima ambao muda mwingi huwatumia watoto wao kuchunga mifugo na shambani jambo lililokuwa likisababisha utoro kukithiri.
Mgombawani alisema baada ya wazazi na walimu kukubaliana hivi sasa hali ya ufaulu imeongezeka ambapo nyumba mbili za walimu hutumika kama mabweni ya wanafunzi kwani watoto wa kiume huishi na mwalimu wa kiume ilihali wanafunzi wa kike wakiangaliwa na mwalimu wao hapo hapo shuleni.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Magwalisi, Moses Fute alisema kipindi hicho cha masika wazazi hutumia kuwatuma watoto wao shambani na kuchunga ng’ombe badala ya kuwapeleka shule hivyo njia ya kunusuru hali hiyo ni serikali kujenga madaraja ili kupitike katika kipindi chote cha mwaka kwani walimu hulazimika kutembea kilomita 30 kutoka Mji wa Rujewa.
Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Jonathan Chengula alisema licha ya ushirikiano anaoupata kutoka kwa walimu, wazazi na uongozi wa Kamati ya Shule na vitongoji, lakini anakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja na walimu

No comments:

Powered by Blogger.