MBARAKA AWAITA SIMBA MEZANI
MuroTv
Mbaraka awaita Simba mezani
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Simba, Zacharia Hans Pope
“Nipo tayari kurudi Simba endapo watakidhi mahitaji yangu kwa maana mkataba wa awali ulimalizika ndio maana Kagera Sugar wakanichukua,” alisema. Mbaraka alisema alitolewa kwa mkopo Kagera Sugar na Simba, lakini baada ya mkataba wake na Simba kumalizika akasajiliwa na Kagera Sugar mpaka sasa tofauti na Simba wanavyodai bado ni mchezaji wao halali.
“Mimi ni mchezaji halali wa Kagera Sugar kwani mkataba wangu na Simba ulishamalizika kwa hiyo kama wananihitaji inabidi tukae chini na kuzungumza,” alisema Mbaraka. Pia Mbaraka alisema malengo yake katika msimu uliopita ni kuwa mfungaji bora, lakini hakufanikiwa badala yake akaishia kufunga mabao 12 lakini atahakikisha lengo lake linatimia msimu ujao.
Mbaraka amepata tuzo ya mchezaji bora chipukizi katika msimu wa ligi 2016/2017. “Nilipanga niwe mfungaji bora msimu huu, lakini kwa bahati mbaya malengo yangu hayajatimia, nashukuru kwa hii tuzo niliyoshinda ya mchezaji bora chipukizi,” alisema

No comments:
Post a Comment