ABDUL BOSI MPYA AZAM
MuroTv
Abdul bosi mpya Azam
31 Mai 2017
Aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba
Habari za uhakika kutoka Azam jana zilisema, Kawemba aliyekuwa na mkataba wa miezi sita Azam amemaliza mkataba wake jana na uongozi wa Azam haukumuongeza.
Akizungumza na gazeti hili, Abdul Mohamed ambaye awali alikuwa Meneja Mkuu alikiri kutokea kwa mabadiliko hayo ya uongozi na kuomba ushirikiano kwa wadau wa Azam. “Ni kweli kuna mabadiliko hayo ya kiuongozi, naahidi kufanya kazi kwa weledi kuipatia Azam mafanikio, naomba ushirikiano tu kwa wadau wa soka na Azam kwa ujumla,” alisema.
Kabla ya kuwa Azam, Abdul alifanya kazi katika kituo cha redio Clouds Fm na Shirika la Utangazi Uingereza (BBC). Azam iliyokuwa moto wa kuotea mbali kwa miaka minne iliyopita, msimu huu haikuwa vizuri kama ilivyotarajiwa na ilimaliza Ligi Kuu msimu wa 2016/2017 ikiwa nafasi ya nne.
Aidha timu hiyo, iliyoshiriki michuano ya kimataifa kwa miaka mitatu mfululizo, sasa haitashiriki mwakani baada ya kukosa kombe la FA na ubingwa wa Ligi Kuu.
No comments:
Post a Comment