MALI WAMEINGIA FAINALI YA AFCON U-17 KWA MARA NYINGINE TENA
Michezo
PICHA 6: Mali wameingia fainali ya AFCON U-17 kwa mara nyingine tena


Mali ambao ndio mabingwa watetezi wa Kombe hilo walilofanikiwa kutwaa mwaka 2015 katika ardhi ya Niger wamefanikiwa kupata ushindi wa penati 2-0 dhidi ya Guinea, hiyo ni baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare tasa na mikwaju ya penati ikaamua mshindi.

Ushindi wa Mali kwa kiasi kikubwa umechangiwa na golikipa wao Youssouf Koita ambaye amefanikiwa kucheza penati tatu za Guinea wakati moja ikitoka nje, ushindi huo sasa unaifanya Mali kucheza mchezo wa fainali dhidi ya timu ya taifa ya Ghana May 28 wakati Guinea atacheza na Niger kutafuta mshindi wa tatu.



Shabiki wa Mali aliyevamia na kuingia uwanjani kwa ushindi wa timu yake.

No comments:
Post a Comment