BREAKING: Kenyatta atangazwa rasmi kuwa mshindi wa urais Kenya
Bw Wafula Chebukati amemtangaza Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumanne.
Bw Kenyatta alipata kura 8,203,290 na angalau asilimia 25 ya kura katika kaunti 35.
Mwenyekiti huyo amekabidhi cheti cha ushindi kwa Bw Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati ametangaza matokeo ya uchaguzi wa urais kama ifuatavyo:
Jumla ya wapiga waliojiandikisha 19,611,423
- Ekuru Aukot 27,311 (0.18)
- Abduba Dida 38,093 (0.25)
- Cyrus Jirongo 11,705 (0.08)
- Japheth Kaluyu 16,482 (0.11)
- Uhuru Kenyatta 8,203,290 (54.27)
- Michael Wainaina 13,257 (0.09)
- Joseph Nyagah 42,259 (0.28)
- Raila Odinga 6,762,224 (44.74)
No comments:
Post a Comment