Mbinu za Kuongeza Kipato Kwa Asilimia 100 ya Kipato Chako cha Sasa
Na Prosper Muro
Suala la kuongeza kipato ni la msingi sana na lina umuhimu mkubwa kwa
kila mmoja. Si watu wengi sana duniani wana kipato cha kutosha kutimiza
ndoto zao maishani,wakati mwingine hata kukidhi mahitaji ya msingi kama
chakula,malazi,mavazi ,afya na elimu binafsi na za watoto wao.
Kama ilivyo kwangu binafsi naamini pia kuna umuhimu mkubwa wa
kuangalia namna nyingine tofauti na kile unachokifanya sasa hivi ambacho
kitasaidia kuongeza kipato juu ya kile unachopata sasa.
Mbinu 5 za Kuongeza Kipato Kwa Asilimia 100 au Zaidi ya Kipato Chako cha Sasa
Zifuatazo ni mbinu 5 ambazo zinaweza kumsaidi kila mmoja anayetaka kuongeza kipato chake
1. Anzisha Biashara yenye Mahitaji kwa Jamii
Zig Ziglar ,Mwandishi wa vitabu na mwanamasoko maarufu duniani anasema “ukiwasaidia watu wengi kupata wanachotaka nawe pia utapata unachotaka”. Kwa
maana nyingine ni kwamba ukitaka kufanikiwa kiuchumi basi tafuta nini
watu wanataka na tengeneza bidhaa au toa huduma kujaza mahitaji hayo ya
watu.
Kwahiyo unaweza kuongeza kipato
chako kwa kuanzisha biashara inayotoa suluhisho la matatizo ya watu au
huduma inayohitajika na watu.
Kama watu wanahitaji kupunguza uzito
kutokana na hatari za kiafya hivyo wangependa kupata suluhisho ya
tatizo lao,hivyo unaweza ukaanzisha huduma ya mazoezi kwa kuanzisha
nyumba ya mazoezi pamoja na kuweka walimu wa kuwasidia wateja wako.
Wateja wanaweza kujisajili na kulipa ada ya mwaka ya uanachama ili
kuhudhuria mazoezi au wakalipa kila wanapohudhuria.
Au unaweza ukaanzisha duka la
vyakula vyenye kujenga afya njema kama mbogamboga na unga wa nafaka
zisizokobolewa,mafuta yasiyo na rehemu nyingi kama alizeti na ufuta na
vyakula vingine visivyo na madhara kwa afya za watu.
2. Ingia katika Biashara ya Mtandao
Biashara hizi zimeshamiri sama
barani Amerika na Ulaya na kwa sasa hivi zimeingia mabara mengine
ikiwemo Afrika. Mfumo huu wa biashara unampa mtumiaji na msambazaji
faida mara mbili, kwanza faida ya kutumia bidhaa yenyewe na ya pili ni malipo yatokanayo na kuwajulisha wengine kuhusu biashara na kujiunga na matumizi yao ya bidhaa ya kampuni husika.
Watu wengi wana matazamo hasi na aina hii ya biashara, ni wazi
kwakuwa watu hawana elimu ya kutosha kuhusu mfumo huu ni kitu cha
kawaida kuwa nahofu -inaitwa “hofu ya usichokijua”. Kitu cha msingi ni kupata elimu kwanza ya namna mfumo huu ilivyo. Ukitaka kujua zaidi tuandikie barua pepe au tupigie simu.
Ili kuongeza kipato amua kujifunza
bishara ya mtandao na kama ilivyo katika kujifunza chochote njia rahisi
ya kufanikiwa ni kufanya kwa vitendo. Chagua kampuni yenye bidhaa nzuri
itakayokufaa na itakayofaa wengine pia na ujiunge. Pia angalia kampuni
yenye mfumo mzuri wa malipo.
Mwanafalsafa wa biashara na tajiri mkubwa duniani siku za nyuma John D. Rockefeller alisema “Ni bora kupata 1% toka kwa watu 100 kuliko kupata 100% toka kwa mtu mmoja”.
Biashara ya mtandao inasimama katika falsafa hii. Unahitaji kuwa na
timu ya watu kadhaa ( 10 kwa mfano) ambao nao wataongea na wengine na
mapato yako na yao yatategemea kazi ya ujumla wao. Unatumia nguvu kidogo
kupata kipato kikubwa.
Katika mfumo wa kawaida wa kufanya
kazi kama biashara ya kuuza nguo mfano au vifaa vya ujenzi, juhudi ni ya
mtu mmoja, ili uongeze mapato unatakiwa kuanya kazi muda mwingi zaidi.
Baadhi ya biashara za kujiunga leo ni: Forever Living Products,OneCoin na Trevo
Binafsi ninafanya Trevo na Rifaro unaweza kusoma zaidi hapa:
Trevo: www.trevonetworkarketing.com Rifaro: www.bongoposts.com/rifaro
Binafsi ninafanya Trevo na Rifaro unaweza kusoma zaidi hapa:
Trevo: www.trevonetworkarketing.com Rifaro: www.bongoposts.com/rifaro
3. Ongeza Mtandao wa Watu na Mahusiano
Unaweza kuongeza kipato chako kwa
kujenga mtandao na watu mbalimbali na kisha kuwajulisha biashara
unazofanya. Wataalamu wa masoko wanasema watu hawanunui bidhaa au huduma
yako unayotoa bali wananua mahusiano. Kwa maana kwamba watu ili wanunue
bidhaa yako au huduma ni lazima wawe na mhusiano mazuri na wewe kwanza.
Mahusiano haya yanaweza kuwa yamejengwa kwa muda mrefu au katika dakika
chache mtu alipoingia dukani kwako.
Vitu 3 vinavyomfanya mtu anunue bidhaa yoyote:
Imetambulika kuwa ili mtu anunue kitu vifuatavyo ni vitu muhimu
- Utaalamu: Aamini kuwa wewe mtoa huduma ni mtaalamu katika eneo hilo
- Urafiki: Mahusiano yenu ni mazuri yani umejenga urafiki mfano kwa huduma kwa mteja unyoionesha na lugha nzuri unayotumia kwa mteja, watu wanannnua toka kwa watu wanaowapenda
- Uaminifu au Imani: Mtu anayenunua ni lazima aamini kuwa mtu anayempa huduma ana uwezo na ni mkweli.
Mambo haya matatu ni muhimu sana kusaidia kufanikiwa katika utoaji wa huduma na mapato ya biashara unayotoa.
4. Tangaza Biashara Zako katika Mtandao
Matangazo ya biashara ni muhimu sana
ili kuwafikishia habari watu wengi. Kuna aina nyingi za kuweza
kutangaza biashara kama redio,TV na magazeti lakini hapa tutaangalia
aina mpya na yenye nguvu kubwa ya matumizi ya mtandao wa intaneti.
Imefahamika kuwa takribani watu bilioni 3 (Kulingana na taarifa toka mtandao wa internetworldstats.com Nov 2015)
wapo katika intaneti kwa maana ya kuwa watu hawa wanatumia mtandao wa
intenet aidha kwa mawasiliano,burudani au biashara. Katika hawa wengi
wapo katika mamitandao ya kijamii kama facebook Bilioni 1 , Twitter
Milioni 400 na Instagram Milioni 100.
Kama unataka kuwafikia watu wengi zaidi duniani basi mtandao wa intaneti ni sehemu ya kufikiria kwanza.
Baadhi ya matangazo katika intaneti
yanalipiwa. Na mengine ni bure. Andaa matanzano ya video na weka katika
mitandao ya facebook,youtube na picha katika mitandao ya picha kama
intragram an pinterest.
Tovuti na blogu ni kitu kingine ambacho ni muhimu sana nadiriki kusema cha lazima katika karne hii ya habari.
Bill Gate (Tajiri namba moja Duniani kwa muda mrefu) aliwahi kusema “Kama biashara yako haitakuwa katika intaneti basi biashara yako itakufa” akiwa
na maana kuwa ni muhimu sana kwa biashara yoyote kujitangaza na kuwo
katika mtandao wa intaneti katika karne hii ya digitali. Watu
wataendelea kuwa digitali zaidi na huduma nyingi zitakuwa katika
mtandao.
Inatabiliwa kuwa katika karne ijayo
hata hela zitakuwa katika mfumo ywa kadi na eletroniki tu. Unaweza kuona
haya yameshaanzakutokea. Kadi za plastiki zinatumika kununua huduma
mbilimbali na huduma za kieletroniki kama “mobile money” na “web wallet” ambapo huhitaji hata kuwa na kadi wala pesa taslimu kufanya miamala.
Hivyo ili kuoneza kipato tangaza huduma unazitoa kupitia mtandao na jenga biashara yako katika mtandao
Ukitaka habari zaidi kuhusu
kutengeneza tovuti na kuiweka biashara yako katika mtandao kwa gharama
ndogo pata msaada kwa kuwasiliana na Absolute Solutions Ltd – Bofya Hapa
5. Ongeza Elimu na Utaalamu katika Kazi
Unaweza kuongeza kipato zaidi kwa
kuboresha kili unachofanya sasa. Mfano kama wewe umeajiriwa basi unaweza
kupata malipo zaidi kwa kukuza ujuzi wako na kupandishwa cheo na
kulipwa mshara mkubwa zaidi.
Jenga uwezo wa kuweza kufanya vizuri zaidi na kuzalisha zaidi ili kuweza kupata malipo maradufu.
Anza kozi katika muda wa jioni au
kozi ya mbali. Lakini uanaweza kwenda chuoni na kusoma kwa masaa yote
kama unaweza kupata ruhusa hiyo kazini kwako.
Kama umejiajiri na unafanya bishara
binafsi ni muhimu kujifunza kitu kipya na kupata taaluma zaidi ambayo
itakusaidia kuboresha biashara yako na kuongeza mapato.
Mwisho
Natumaini makala hii itakusaidia
katika maamuzi yako kuhusu kuongeza kipato kwa asilimia 100 ya kile
unachopata sasa na kuboresha maisha tako na familia yako.
Tafuta matatizo ambayo watu wanayo
na yanahitaji ufumbuzi,buni na jenga suluhisho litakalowasaidia watu na
matatizo yao na utafanikiwa kuongeza kipato chako wakati ukiwasaidia
watu katima matatizo yao.
Je unafahamu mbinu nyingine ambazo zinaweza kusaidia kuongeza kipato? basi tuandikie hapa chini katika kisanduku cha maoni.
Na kama umeipenda makala hii basi bonyeza vitufe hapo chini na washirikishe watu wengine ili wafaidike pia
Asante sana kwa kusoma hadi mwisho
-----Prosper Muro----
No comments:
Post a Comment