Tujikumbushe September 11, 2001 Marekani
Siku hii hujulikana kama September 11 ambapo magaidi 19 wa Kundi la Al-Qaeda wakiongozwa na mshukiwa namba moja Osama bin Laden waligawanyika katika ndege nne ambapo katikati ya safari waliziteka ndege hizo kwa lengo la kufanya shambulizi.
Ndege mbili kati ya hizo zilielekezwa na kugonga majengo mawili marefu yanayotazamana yaliyoitwa ‘Twin towers’ katika kituo cha Biashara cha Dunia ‘World Trade Center ama WTC’ katika mji wa New York ambapo muda mfupi baada ya mlipuko yaliporomoka.
Ndege ya tatu ilielekezwa katika Makao Makuu ya Idara ya Ulinzi Pentagon lakini ndege ya nne haikufanikiwa kufika sehemu iliyolengwa na badala yake ilikwenda kulipuka katika mji wa Pennsylvania.
No comments:
Post a Comment