Usiku wa August 27 2017 Bondia mwenye sifa ya kutopoteza pambano hata moja
Floyd Mayweather alirudi ulingoni kucheza pambano la 50 dhidi ya
Mc Gregor hiyo ikiwa ni muda umepita toka apigane na
Manny Pacquiao na kumpiga.
Mc Gregor ambaye alionekana kuwa na tambo alipigwa na
Mayweather kwa
Technical Knock Out (TKO) round ya 10 pambano la round 12, huo ukawa ni mwisho wa tambo zake dhidi ya
Mayweather, licha ya kipigo hicho
Mc Gregor kupanda tu ulingoni kulimfanya aingize dola milioni 100 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 200 za kitanzania.
Jana September 10 2017
Mc Gregor anayetokea
Ireland ameonekana akiwa amekodi boti binafsi akiwa na familia yake wanaendelea kula bata
Hispania katika fukwe za
Ibiza, kitu ambacho wengi wanaamini anatumia au ana furaha kuingiza Dola milioni 100 licha ya kupoteza.
No comments:
Post a Comment