Header Ads

Mungu ni Mwema!! Takwimu, Listi na Idadi ya Nchi zinazoongoza Kutazama Muro TV blog Mwezi Agosti-September

  Takwimu Muro TV
Wapendwa ni miezi mitatu sasa imetimia tangu blogi hii  (murotv.blogspot.com  na Muro TV) ianzishwe hapo mwishoni mwa mwezi wa Sita mwaka huu wa 2017 chini ya mmiliki ndugu Prosper Alphonce Muro alimaarufu kama Mr Muro akiwa Chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino (St Agustine University of Tanzania) 
Mr Muro
Blogi hii ilianzishwa kwa malengo ya kukuza tasnia ya Habari na Muziki ndani na nje ya Tanzania, ililenga hasa kutoa habari mbali mbali kama vile Michezo, Siasa, Burudani na kuwezesha watu kupata miziki mipya kwa wakati bilakujali ugumu na changamoto mbali mbali zilizopo hasa za Kifedha na Vifaa vya kazi.

Leo Tarehe 19 Sept 2017 Tunapenda kuchukua nafasi hii kumshukuru M/zi Mungu kwa pumzi hii na uzima huu aliotujalia hadi leo hii tukiwa wazima wa afya, tunatumaini u mzima wa afya pia msomaji wetu sifa na shukrani zimuendee M/zi Mungu

Pia tunapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru sana wasomaji wetu wote katika pande zote za Dunia na wote waliotupa sapoti yao kutufikisha hapa tulipofikia sasa M/zi Mungu awabariki sana sana hatuna cha kuwalipa ila M/zi Mungu atawalipa mara dufu.

Pia na wote mliotupa changamoto ya aina yoyote ile tunawashukuru  kwani changamoto zenu zimetusaidia  kutambua ni wapi penye makosa na kufanyiwa marekebisho, pia zimetusaidia  kukuza imani ya kile tunachokiamini (Kwamba hakuna mafanikio bila Changamoto)

Tunashukuru sana kwa hatua tulioifikia mpaka sana kwani blogi hii imepata kufahamika nchi mbali mbali hasa nchini Tanzania, pia tunatoa shukrani zetu za dhati nchini Kenya kwani mmeonyesha upendo wa dhati sana kwenye kazi zetu, tunaishukuru sana Anyoula FM hasa kupitia kipindi cha Bazuka Show kikiongozwa na King Davy & Queen Anna kwani imetusaidia sana kufahamika nchini Kenya na nchi zingine kama vile Oman, Aislandi, Uholanzi, Ureno, Burundi, India, Indonesia  na Marekani (May God Bless You).

Tumetoa Takwimu za hadhira za 19 Agosti- 19 September 2017 kuonyesha maendeleo ya blogi hii kwa mwezi na kuwashukuru wapenzi wasomaji wetu kwa ushirikiano wenu mnaoendelea kutupatia kwani tunatambua sana mchango wenu kwetu.

Hapo chini tumeambatanisha Listi ya Nchi kumi (10) zilizoonyesha ushirikiano wa dhati kwetu kuanzia 19 Agosti- 19 Septenber zikiongozwa na Tanzania, Kenya, Indonesia, Marekani, Uholanzi, Ureno, Aislandi, Burundi, Oman na India.

LIST YA NCHI ZINAZOONGOZA MURO TV




Kwa yeyote anaependezwa kufanya kazi na sisi anakaribishwa sana kwani mchango wako na shea yako itatambulika kama mmoja wa wanafamilia ya Muro TV na murotv.com
Pia kwa yeyote mwenye mchango wa aina yoyote ile iwe kimawazo, kiuchumi n.k anakaribishwa sana kwani lengo letu ni kufika mbali zaidi.

TANGAZA NASI
Tangaza biashara yako kwa gharama nafuu iwafikie zaidi ya wasomaji wetu 50000 kwa siku.
Kwa mawasiliano 
Piga simu nambari- 0768-786-851 
Email- murotv1@gmail.com

No comments:

Powered by Blogger.