Header Ads

RAILA ODINGA ATANGAZA KUTOSHIRIKI UCHAGUZI WA MARUDIO

Siku chache baada ya Mahakama ya Juu Kenya kuamuru Uchaguzi Mkuu wa Urais urudiwe kiongozi wa upinzani Raila Odinga ametangaza kutokuwa tayari kushiriki marudio ya uchaguzi huo uliotangazwa kufanyika October 17, 2017.
Licha ya kufungua kesi Mahakamani kupinga matokeo ya Uchaguzi wa August 8, 2017 uliompa ushindi Uhuru Kenyatta, Odinga ametaka kuwepo mikakati ya kisheria na kikatiba inayohitajika, kabla hajakubali kushiriki uchaguzi huo.
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Kenya, September 4, 2017 ilitangaza marudio ya Uchaguzi Mkuu wa Urais yatafanyika October 17, 2017 baada ya agizo la Mahakama ya Juu kutaka uchaguzi urudiwe ndani ya siku 60.

No comments:

Powered by Blogger.