Header Ads

UMATI WAFURIKA KUIMBA PAMOJA NA ALIKIBA

 http://xclusive.co.ug/wp-content/uploads/2016/12/Singer-Ali-Kiba-shaking-hands-with-his-fans.jpg
Mkali wa Bongofleva Tanzania Alikiba baada ya kuachia wimbo wake #Ceduse Me na kuwa gumzo sana Mitaani na Mitandaoni baada ya kuvunja Rekodi ya kuwa na Views Millioni Moja ndani ya Masaa 38 tangu alipoachia Video yake Mpya inayotamba kwa jina hilo la Ceduse Me
Amekuwa akiwashukuru watanzania pamoja  na wanaafrika Mashariki kwa Sapoti wanayompa, Leo Agosti 31 amewatembelea wakazi wa Mbagala Jijini Dar es Salaam na kufanya Show yake ya kwanza tangu alipoachia wimbo huo
Watu wamefurika si kawaida na kuimba wimbo huo mwanzo mwisho kitu ambacho ni chakushangaza kwani wimbo huo una takribani siku sita tu tangu ulipotoka.
Alikiba ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwashukuru wakazi wa Mbagala kwa wingi wao na upendo waliouonyesha kwake.
  • officialalikibaNingependa kuwafikia wote kutoa shukurani zangu na nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kuwafikia wengi wenu .. Mbagala nimefurahi sana kukutana na nyie leo na ahsanteni kwa kuupokea ujio wangu wa #SeduceMe na kwa @cloudsfmtz #XXL kwa kunipa nafasi hiyo.Endelea kuangalia #SeduceMe on my Vevo account, link kwenye bio.
    #Rockstar4000
    #KingKiba



ANGALIA VIDEO

No comments:

Powered by Blogger.