Rais, Magufuli ampiga biti Mbunge Cuf.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
amempiga biti Mbunge na viongozi wa upinzani mkoani Tanga kutojisifia
kuwa wao wameleta mradi wa Bomba la Mafuta katika eneo la Chongoleani
Tanga.
Rais
Magufuli amesema kuwa asitokee mtu yoyote katika jimbo hilo na kusema
kuwa mradi huo wa bomba la mafuta ameuleta kwani mradi huo umeletwa na
serikali ya Magufuli chini ya Chama Cha Mapinduzi.
“Hili bomba la mafuta lingeweza kwenda kokote hapa Tanga,
tungeweza kulipeleka hata katika majimbo mengine ambayo yapo chini ya
CCM lakini tumelileta hapa Chongoleani, sijui hata chama gani kwa sababu
serikali yangu haibagui chama inataka kuleta maendeleo ya wananchi,
hivyo tumeleta hili bomba la mafuta hapa ili kuleta maendeleo kwa
wananchi asitokee mtu yeyote akasema amelileta hili bomba, ashindwe na
alegee, limeletwa na serikali ya Magufuli” alisema Rais Magufuli.Aidha Rais Magufuli na Rais wa Uganda Museveni leo tarehe 5 Agosti 2017 wameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima, Kaskazini mwa Uganda hadi Chongoleani Tanga.
Kata ya Chongoleani Tanga ipo katika Halmashauri ya Tanga Mjini, jimbo ambalo lipo chini ya Mbunge Mussa Mbaruk kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF)
No comments:
Post a Comment