Header Ads

"Ni Bora Niache Muziki" - Nick Wa II

 http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2014/05/Nikki-wa-Pili_2.jpgSiku ya August 26, 2017 msanii wa rap nchini Nikki wa pili aliweka post yake kwenye ukurasa wa Twitter na kuandika maneno yaliyosomeka…>>>“Kuguswa kwa nyavu za degea kutasubiriwa kama upinzani kuingia ikulu” kitu kilicho mfanya shabaki kutoa maoni yake kuhusu hilo.

Shabiki alikuja kukoment chini kwa kumpa ushauri wa kuacha kufanya siasa bali afanye muziki licha ya kuwa anawawakilisha wasanii kwa waziri wa habari, waziri Mwakyembe na  shabiki huyo aliandika...>>>”Acha siasa kafanye muziki… Ndilo unalo liweza. Don’t get twisted kwakua umekua muwakilisha wasanii kwa mwakyembe” – Shabiki
Nikki wa Pili ikabidi amjibu shabiki huyo kwamba yupo tayari kuacha muziki na kufanya siasa maana muziki hauwamui maisha wakati siasa ni sehemu ya maisha ya watanzania…>>>“Bora niache muzik maana muzik hau amui maisha ya watanzania, siasa ni maisha yangu na kila mtanzania ninaye mjuwa na atakaye kuja” – Nikki wa Pili

No comments:

Powered by Blogger.