Nawal baada ya kuachana na Nuh Mziwanda na kuolewa na mwanaume mwingine (+Audio)
Kupitia kipindi cha The Weekend Chat Show August 4, 2017 kinachorushwa na Clouds TV, aliyekuwa mke wa Mwimbaji Nuh Mziwanda, Nawal amefunguka na kuelezea kuhusu mume wake mpya aliyefunga naye ndoa hivi karibuni.
Nawal ambaye amekiri kuachana na Nuh na kufunga ndoa na mwanaume mwingine amesema ameolewa kwa sababu mume huyo ameona kuwa anafaa kuwa mkewe ambaye anamjali pamoja na familia yake.
>>>”Tumekutana hivyo hivyo kwani Nuh tulikutana naye vipi? Kwanza mwanaume aliyenioa ameniona nafaa kuwa mke na kuniweka ndani siyo wa kunichezea. Nimemuona ni mwanaume anayejali familia yangu, anamjali sana mwanangu kushinda hata mimi mwenyewe.
“Yaani nikikohoa tu kumwambia mwanangu hana kitu fulani, kama umeme analeta. Kwa hiyo, nimeona ni mwanume anayenifaa. Ni wanaume wachache sana wanaopenda watoto ambao si wa kwao.
“Bwana namjua vizuri sana nimeolewa, nimesitirika, nimewekwa ndani. Kazi ya mwanamke kuhudumiwa kukaa ndani na kuletewa. Rangi siyo ya kujishughulisha kukimbizana na majungu nikaungua na maji ya moto. Mnajua mwanamke ni mvumulivu kuliko mwanaume na ukiona mwanamke kaachia ngazi basi jua kabisa yamemfika hapa.” – Nawal.
Msikilize zaidi hapa Nawal akifunguka zaidi kuhusu ndoa yake mpya…
No comments:
Post a Comment