Header Ads

Mume kamuwekea mkewe sumu kwenye maji ya kunywa…kisa?

  Leo August 1, 2017 kupitia Hekaheka ya Leo Tena ya Clouds FM mtangazaji Geah Habibu ameifuatilia hii stori ya mwanaume ambaye anadaiwa kumuwekea mkewe sumu kwenye chakula kwa ajili ya mwanamke mwingine.
Indaiwa kuwa mwanaume huyo alimchoka mke wake waliyeishi naye kwa miaka Kumi na kubahatika kupata watoto huku akiwa na mwanamke mwingine aliyekuwa anaishi Uarabuni ambaye alimtolea mahali kwa ajili ya kufunga naye ndoa.
Baada ya kugundua kuwa mumewe alikuwa na mwanamke mwingine, mke huyo alimtafuta na kumuonya lakini mwanamke hakuonesha kushtuka ambapo mumewe alipotambua alimuwekea sumu kwenye maji ya kunywa na kupoteza fahamu baada ya kuyanywa.

No comments:

Powered by Blogger.