Korea Kaskazini yamwachilia mchungaji aliyetaka kupindua serikali
Mchungaji ambaye
alihukumiwa kifungo cha maisha jela na kazi ngumu nchini Korea Kaskazini
kwa kutekeleza uhalifu dhidi ya taifa hilo mnamo mwezi Disemba 2015
amewachiliwa huru kulingana na chombo cha habari cha taifa hilo.
Taarifa
imethibitisha kwamba kiongozi huiyo wa dini mwenye umri wa miaka 62
Hyeon Soo Lim alikuwa ameachiliwa kutokana na mahitaji ya kibinaamu.Siku ya Jumanne serikali ya Canada ilithibitisha kwamba ujumbe uliwasili mjini Pyongyang ili kuzungumzia kuhusu kesi ya bwana Lim.
Kuwachiliwa kwake kunajiri wakati ambapo kuna wasiwasi kati ya Marekani na Pyonyang.
Mchungaji huyo mwenye makao yake huko Toronto ambaye anadaiwa kuwa na mizizi ya Korea Kusini alikiri hadharani kwamba alikuwa na njama ya kutaka kuipindua serikali ya Korea Kaskazini na kuanzisha taifa la kidini.
Familia ya bwana Lim ilisema kuwa alisafiri hadi Pyongyang mnamo mwezi Januari 2015 ili kujenga nyumba ya kuwaangalia watu wazee pamoja na watoto mayatima.
Kanisa lake lilithibitisha kuwa ameitembelea nchi hiyo kwa zaidi ya mara 100 tangu 1997.
Kwa sababu vitendo vya kidini vimepigwa marufuku nchini Korea Kaskazini , mamlaka mara nyengine huwakamata raia wa kigeni kwa maswala ya kidini, na visa kama hivyo vimeshuhudia wafungwa kukiri hadharani.
Katika mahojiano na CNN mnamo mwezi Januari ,bwana Lim alielezea kuhusu kifungo chake na kazi ngumu.
Alisema kuwa alilazimika kuchimba mashimo saa nane kwa siku katika kambi ambayo hakuona mfungwa mwengine yeyote.
Mnamo mwezi Januari mwanafunzi wa Marekani Otto Warmbier alifariki siku sita baada ya kurudishwa nchini kwao kutokana na mahitaji ya kibinaadamu kutoka katika jela za korea Kaskazini.
No comments:
Post a Comment