Barcelona yamshtaki Neymar kwa kuhamia PSG
Barcelona
imesema inamshtaki aliyekuwa mshambuliaji wake Neymar kwa kitita cha
£7.8m kufuatia uhamisho wake katika klabu ya PSG nchini Ufaransa.
Mchezaji
huyo wa kimataifa kutoka Brazil alivunja rekodi ya uhamisho kwa kitita
cha £200m kwa timu hiyo ya Ufaransa mnamo mwezi Agosti baada ya
kununua kandarasi yake katia klabu ya Barcelona .Barcelona sasa inamtaka kurudisha marupurupu aliyopewa baada ya kutia saini kandarasi mpya ya miaka mitano miezi tisa pekee kabla ya kulazimisha uhamisho huo.
''Klabu inataka mchezaji huyo kurudisha marupurupu aliyolipwa kwa kuwa hakumaliza kandarasi yake'', ilisema taarifa.
Mbali na Yuro milioni 8.5 za marupurupu, klabu hiyo pia inataka kulipwa asilimia 10 ya fedha hizo kwa kuchelewa kulipwa.
Kufuatia uhamisho huo Barcelona ilitangza kuwa inazuilia Yuro milioni 26 za marupurupu ambazo mchezaji huyo alifaa kulipwa.
No comments:
Post a Comment