Header Ads

Changamkieni fursa Mradi wa Bomba la Mafuta – Dkt. Pallangyo

Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana
Pallangyo amewataka wananchi wanaoishi katika mikoa itakayopitiwa na
miundombinu ya bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini
Uganda hadi katika Bandari ya Tanga nchini Tanzania kuchangamkia
fursa mbalimbali zitakazojitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi.

Dkt.
Pallangyo aliyasema hayo mapema jana jijini Dar es Salaam kupitia
kipindi maalum cha 360 kilichorushwa na kituo cha televisheni cha Clouds
wakati akielezea maandalizi ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa bomba la
mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania
unaotarajiwa kufanyika Agosti 05, mwaka huu.

Alisema kuwa
wananchi katika maeneo husika wanatakiwa kujiandaa kwa ajira wakati wa
maandalizi na utekelezaji wa mradi, ikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma
mbalimbali za vyakula, usafiri na ufundi.

“Fursa zitakazokuwepo
ni nyingi mno, vijana waliomaliza Vyuo vya Ufundi wataweza kufanya kazi
za uchomeleaji wa vyuma, madereva wenye leseni kupata kazi, wakina mama
lishe kuuza vyakula, wakulima kuuza mazao kwa walaji watakaoongezeka
kutokana na uwepo wa mradi huo, alisema Dkt. Pallangyo.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari na mwongozaji wa kipindi cha 360 cha Clouds TV, Hassan Ngoma katika mahojiano maalum kuhusu uzinduzi wa mradi wa wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania unaotarajiwa kufanyika Agosti 05, mwaka huu yaliyofanyika mapema Julai 31, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Mwandishi wa habari na mwongozaji wa kipindi cha 360 cha Clouds TV, Hassan Ngoma akiuliza swali kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) kwenye mahojiano hayo.

No comments:

Powered by Blogger.