BREAKING: Maamuzi mapya ya Mahakama Kuu kesi ya Wabunge 8 waliofutwa CUF
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es
Salaam leo August 4, 2017 imetupilia mbali pingamizi la Wabunge 8 wa
Viti Maalumu waliofutwa uanachama na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi
CUF Prof. Ibrahim Lipumba ya kutaka wabunge wateule 8 wasiapishwe na
Bunge.
Uamuzi huo, umetolewa na Jaji Lugano Mwandambo ambaye amesema ametupilia mbali pingamizi hilo la zuio la kuapishwa kwa Wabunge hao 8 na kwa mantiki hiyo, Wabunge wapya walioteuliwa kuziba nafasi zao wanaweza kuapishwa.

No comments:
Post a Comment