ENEKA YA DIAMOMD PLUTNUMZ KUFANANA NA FALL YA DAVIDO-LAIZER
Siku chache baada ya mwimbaji wa Bongofleva na kiongozi wa WCB, Diamond Platnumz kuachia video ya wimbo mpya ‘Eneka’ mashabiki na wafuatiliaji wa muziki wa Bongo wanadai kuwa wimbo huo unafanana na wimbo wa mwimbaji staa wa Nigeri Davido unaoitwa ‘Fall’.
Kutokana na stori hizo kushika kasi kwenye mitandao ya kijamii producer ambaye alihusika kutenegeneza wimbo huo kutoka WCB, Lizer ambapo amefunguka kutolea ufafanuzi juu ya madai hayo ya Eneka kufanana na Fall.
>>>”Kwanza naweza nikasema hivi huu ni muzuki na
muziki pia una style yake inategemea ni muziki wa aina gani unaweza
ukafanana. Nimesikia hizo habari kwamba wimbo wa Eneka unafanana na Fall
ya Davido lakini naomba kitu kimoja watu waelewe kwamba muziki wa
Kimarekani umechanganywa na kiafrika lakini vitakavyobadilika
vitabadilika vichache.
“Tusiwe waongo, sisi tunafuata
Nigeria wanafanya nini, tusiwe wanafiki kwamba tusiangalie Nigeria
wanafanya nini kwa sababu wametutangulia. Kwa hiyo ili tufike kule
walikofika wao lazima tupite njia ambazo wanapita wao.
“Sioni ajabu kwamba mtu akisema hii imefanana…mi ninachojali
ni kwamba watu watapokeaje nyimbo, itapendwa au itafanya vizuri. Hicho
ndicho ninachokiangalia zaidi.” – Lizer.
No comments:
Post a Comment