Header Ads

BREAKING: Kupatwa kwa Mwezi Leo tarehe 7 Agosti​

 http://nightskies.org/Archive/ns121710/images/Lunar%20Eclipse%20Diagramlg.jpg
Na Prosper A Muro
Jioni ya leo Jumatatu tarehe 7 Agosti WaTanzania wanaweza kushudia tamasha zuri angani. Hii ni tarehe ambako kupatwa kwa Mwezi kunaleta giza juu ya sehemu ya Mwezi mpevu kwa muda wa karibu masaa mawili.

https://wordlesstech.com/wp-content/uploads/2011/12/Images-of-the-Lunar-Eclipse-Dec.-10-5.jpg
Tukio hili limeanzatokea mapema leo jioni ya Jumatau kuanzia saa mbili na nusu hivyo ni wakati mzuri wakuangali kwa vile watu bado wapo macho na wanaweza kuiangalia wakitoka tu nje na kuangalia angani upande wa mashriki. Ni nafasi nzuri kwa waalimu kuwaeleza wanafunzi wao tukio hili kabla na kulijadili pamoja nao baada ya tukio. Pia kupatwa kwa Mwezi unaweza kuangaliwa kwa macho moja kwa moja bila madhara kwa vile mwanga wa Mwezi hauumizi na kivuli kinaupunguza hata zaidi.

http://cdn1.collective-evolution.com/assets/uploads/2016/08/lunar-eclipse-aqu-2016-3-759x500.jpg
Tukiangalia anga la jioni siku  ya leo Jumatatu Agosti 7, upande wa mashariki, tunaona jinsi gani Mwezi mpevu ulivyoanza kupaa juu mara baada ya machweo. Mwezi mpevu ni hali ya Mwezi ambako unaonekana kama duara kamili unaong’aa. Kupatwa kwa Mwezi hutokea mara chache wakati Mwezi unapokuwa mpevu.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjqEgDYMv4hJcN9YySL7k2-ZhEw2sbRQAZ0C_T_kdMpsncY7FcvoEQK_HFcydUZOCWgD0fe_iYOSru6j53H7FofwOlV8jRYR_SbhfjxxDt1Jz91uDgHSiQsxHQ_d-d2zazqISnIxjALqb8/s1600/Lunar+Eclipse.jpg
Mnamo saa mbili na dakika ishirini na tatu (2:23) tumeaona jinsi gani dura angavu ya Mwezi mpevu ulivyoanza kuliwa na giza kuanzia upande wa chini kulia . Hadi saa tatu na dakika ishirini (3:20) sehemu kubwa, kiasi robo, ya duara ya chini ya Mwezi utapatwa na giza. Kuanzia hapa giza itapungua hadi mnamo saa nne na dakika kumi na nane (4:18) giza itapotea kutoka kwenye ncha ya juu upande wa kulia.


Ukiendelea kutazama Mwezi utaona ya kwamba itachukua tena muda hadi mnamo saa tano na dakika hamsini (5:50) hadi Mwezi mpevu unaonesha tena nuru yake yote. Sababu yake ni kwamba bado kuna kivuli chepesi kinachoendelea kuziba nuru yake kiasi.


Kupatwa kwa Mwezi kunatokea kwa vile tunajua kwamba Mwezi ni gimba kubwa lenye umbo la tufe linalozunguka Dunia yetu kila baada ya siku 29 na robo. Mwanga tunaouona kutoka kwenye Mwezi ni nuru ya Jua iliyoakisiwa na uso wa Mwezi. Kila wakati nusu moja ya Mwezi inaangazwa na Jua. Kutokana na Mwezi kuzunguka Dunia, mara moja kwa mwezi tunaona uso wake kuwa ni duara ambayo huitwa Mwezi mpevu. Mara nyingine tunaona sehemu tu ulioangazwa na hapa tunaona Mwezi ukiwa robotatu, au nusu, au robo, au hilali. Tunapoangalia upande wa Mwezi usiopokea nuru yoyote kutoka kwenye Jua, hapo tunasema ni Mwezi mwandamo.

https://www.chromosphere.co.uk/wp-content/gallery/lunar_eclipse_20150928/DSC_2547.jpg
http://www.space.com/images/i/000/007/862/original/508898main_wide_corona_eclipse_ti3.jpg?interpolation=lanczos-none&fit=inside|660:*
Kama ilivyo kwa kila kitu kinachoangazwa na nuru kutoka upande mmoja, kunatokea kivuli upande wa pili. Dunia yetu pia huwa na kivuli inapoangazwa na Jua. Kupatwa kwa Mwezi kunaonekana pale ambapo Mwezi unapita ndani ya kivuli cha Dunia. Hapo tunaona kivuli kama giza kwenye uso wa Mwezi mpevu.


Mchoro Kupatwa kwa Mwezi.jpg


Ni vema kujua ya kwamba kuna aina mbili tofauti za kivuli: kivuli kamili na nusukivuli. Kama chanzo cha nuru ni kubwa au pana sehemu ya nuru kutoka pande za pembeni huingia katika kivuli cha gimba. Kwa hiyo kivuli hiki kinakuwa na giza nyepesi ambayo inakuwa pembezoni mwa kivuli kamili.


Hivyo pia inavyotokea wakati wa kupatwa kwa Mwezi. Jua ni gimba kubwa la nuru, na Dunia haitoshi kufunika nuru yote inayotoka kwenye Jua. Nuru kutoka kando ya Jua inaingia kwenye kivuli cha Dunia na kusababisha nusukivuli au kivuli chepsi. Kivuli cha katikati pekee kinakuwa ni kivuli kamili (tazama mchoro).


Kwa hiyo Mwezi unapoanza kupatwa, unapita ndani ya nusukivuli kwa hiyo nuru ya Mwezi inaanza kwa kufifia kidogo. Baada ya hapo Mwezi unaingia kwenye kivuli kamili na unakuwa na uweusi, na mwishoni tena Mwezi unaishia kwa kupita ndani ya nusukivuli, yaani kivuli chepesi. Mwezi ukiwa sehemu ya kati tu ya kivuli ndio tunaona hasa Mwezi umepatwa na kivuli cheusi cha Dunia.


Leo tarehe 7 Agosti  nusukivuli, ilianza kuufunika Mwezi mapema karibu na saa moja, yaani saa 12:50, mara tu baada ya machweo. Kwa hiyo ilikuwa vigumu zaidi kutambua kivuli chepesi kwa vile bado kulikuwa na mwanga wa Jua unaoangaza anga ya upeoni. Kivuli kamili kiliingia karibu saa mbili na nusu (saa 2:23), wakati anga lina giza. Wakati huo, Mwezi tuliona ulianza kuliwa na kivuli cheusi kwa upande wa chini kulia ya Mwezi. Baada ya hapo uweusi uliongezeka hadi kufunika karibu robo ya Mwezi kiasi saa tatu na nusu (yaani 3:20). Robo tu ya Mwezi unaingia ndani ya kivuli kamili. Kwa hiyo tunaona sehemu tu ya Mwezi inafunikwa na uweusi. Uweusi huu utaanza kupungua baada ya hapo, na hadi kufikia karibu saa nne na nusu (yaani 4:18), Mwezi utaachwa na kivuli kamili kwa upande wa juu kulia na uweusi utaisha. Baada ya kupotea kwa uweusi, Mwezi utakuwa ndani ya nusukivuli kwa hiyo nuru yake bado haitakuwa na ukali wa kawaida wa Mwezi mpevu. Hali hii itapungua polepole na uangavu kamili wa Mwezi mpevu utarudishwa ifikapo saa tano na nusu (saa 5:31).
https://www.nasa.gov/sites/default/files/thumbnails/image/superbloodmoon.jpg

Kupatwa kwingine kwa Mwezi kutatokea tena tarehe 27 July 2018 wakati Mwezi wote utafunikwa na kiza kamili. Angalia hapa kwenye intaneti: Eclipses visible in Dar es Salaam, Tanzania - 7 aoû 2017 Lunar Eclipse.


Mapendekezo kwa waalimu

Walimu wanaweza kuchukua nafasi hii kuwaandaa wanafunzi kutazama kupatwa kwa Mwezi nyumbani kwao pamoja na wazazi na ndugu na jamaa, na baadaye kujadiliana nao kuhusu walichoona.


Hapa anaweza kutumia vitabu vya Maarifa ya Jamii darasa la sita ambako kuna habari za kupatwa kwa Mwezi katika somo kuhusu Mfumo wa Jua. Inafaa kuwahi kufundisha habari hizi hata kama somo kwa jumla halikuanzishwa bado.


Hata kwa madarasa ya chini mwalimu anaweza kutumia matini husika.


Wanafunzi wa Sekondari wanaweza kutayarishwa kwa tukio hili kwa kukumbusha walichojifunza katika madarasa msingi na kuunganisha na matini ya somo la Jiografia ya Kidato cha Kwanza inayohusu Mfumo wa Juan pamoja na mada ya kupatwa kwa Mwezi na Jua.


Wanafunzi wa Kidato cha Nne wanaosoma Fizikia katika mada ya Astronomia pia watafaidi sana kufuatilia tukio hili kama elimu nyongeza kwa vile ni muhimu na ya kusisimua, ingawa halipo katika mtala au katika vitabu vyayo. Hii inawahusu pia wanafunzi wa sayansi wote katika Sekondari na Vidato vya Tano na Sita pamoja na wanafunzi wa sayansi vyuoni.


Kwa kila namna mwalimu atachora ubaoni nafasi za Jua, Dunia na Mwezi pamoja na aina za kivuli na kuwaeleza watakachoona wakati Mwezi umepatwa.

Wanafunzi wanaweza kuandika wanachoona wakati wa tukio, wakijibu maswali kama:

- Je waliweza kuona Mwezi?

- Je waliona mabadiliko gani katika uangavu wa Mwezi, tena saa ngapi?

- Giza (au kupungua kwa uangavu) waliona kwenye sehemu gani za Mwezi?

- Wachore sehemu angavu na zenye giza kwenye uso wa Mwezi mpevu.

- Waandike kwa maneno yao jinsi wanavyoweza kueleza walichoona.


Siku ya Jumanne au Jumatano ni nafasi ya kusikia taarifa za wanafunzi, kujibu maswali na kutoa maelezo yanayohitajika.

No comments:

Powered by Blogger.