Header Ads

Ester Bulaya akamatwa na Polisi leo


Moja ya taarifa zinazomake headlines ni pamoja na hii ambayo kuhusu Mbunge wa Bunda Mjini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Ester Bulaya kukamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Rorya katika Mkoa wa Mara akiwa katika majukumu ya kichama.
Bulaya imethibitishwa na Msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene kuwa amekamatwa akiwa akiwa katika Hoteli aliyofikia Tarime ambako alikwenda kwa ajili ya shughuli za kichama.
Tumaini Makene:>>>”Ni kweli tumepata taarifa muda sio mrefu kwamba Mbunge wetu Jimbo la Bunda Mjini ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu Ester Bulaya amekamatwa na Jeshi la Polisi akiwa Hotelini kwake, Tarime. Alikuwa katika shughuli za kichama akiwa kama Mbunge na Mjumbe wa Kamati Kuu.”

No comments:

Powered by Blogger.