Header Ads

Alichokiandika Ommy Dimpoz baada ya video mpya ya WCB iliyotoka baada ya Alikiba


Ijumaa August 25 2017 Mwimbaji Alikiba ameachia video mpya baada ya kimya kirefu ambapo saa kadhaa baada ya kuiachia, WCB pia nao wametoa video yao mpya inaitwa ‘zilipendwa‘ ambapo Diamond amewaongoza vijana wake kama Rich Mavoko na Rayvanny kwenye hiyo video
Muda mfupi baada ya WCB kuachia hiyo ngoma mpya, Mwimbaji Ommy Dimpoz ambae yuko kwenye lebo ambako Alikiba ni mmoja wa Wakurugenzi, amechukua time yake kupost upande maneno ambayo wengi wanahisi ni dongo kwa WCB.
Ommy ameandika mashairi ya wimbo wa zamani ambao wengi waliuimba utotoni >>> Watoto Wangu eeeh!! eeehh!! Mimi Baba Yenu eeeeh!! Sina Nguvu tenaaa Eeeeh za kuua Tembooo
Watoto: Sawa Baba tunakuja kukusaidia Sema itabidi tutumie zilezile mbinu zetu za UJANJA UJANJA si Unajua sikuhizi hayuko peke yake kuna mwingine kajificha
Hayo ni maneno ya Ommy Dimpoz ambapo post yenyewe ni hii hapa chini….. kama hujatazama hizo video mpya za Alikiba na WCB unaweza kuangalia post zilizopita kwenye millardayo.com

No comments:

Powered by Blogger.