Kilichokutwa kwenye Mkojo wa Agness Masogange, Mashadidi Hawakumbuki rangi yake, Mahakamani Leo
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo August 28, 2017 imepokea taarifa ya Mkemia kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali iliyoonesha kuwa sampuli ya mkojo wa Agnes Gerald maarufu kama Masogange una chembechembe za dawa za kulevya.
Taarifa hiyo imepokelewa baada Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kutoa uamuzi wake ambapo amesema Mahakama imepokea taarifa hiyo na pingamizi la utetezi limetupiliwa mbali.
Pingamizi la upande wa utetezi ni kwamba fomu zilizopelekwa kwa Mkemia Mkuu hazikufuata sheria.
Hakimu Mashauri amesema Mkemia huyo Elia Mulima ambaye ni Shahidi wa kwanza ana haki ya kuandaa ripoti, kupima sampuli na kutoa ripoti Mahakamani.
Kuhusu hoja ya kuwasilishwa maombi ya kupimwa mkojo Masogange, Hakimu amesema ni wazi Polisi walipeleka maombi kwa Mkemia na mshtakiwa alienda akiwa chini ya askari wawili, ambapo walipatiwa kontena kwa ajili ya kuweka sampuli ya mkojo wa Masogange.
Mashahidi hawajui mkojo wa Agnes Masogange una rangi gani, Mahakama yaamua
Mkemia kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Elia Mulima leo August 28, 2017 amesema hakumbuki na hafahamu mkojo wa mrembo wa Bongo Agnes Gerald maarufu Masogange una rangi gani.
Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula, Shahidi huyo amesema anamfahamu Masogange baada ya kufikishwa kwenye ofisi za Mkemia, ambapo alimuona majira ya saa 8 mchana na kueleza kuwa alipokea sampo ya mkojo wa Masogange kutoka kwa Detective Copro Sospeter baada ya kumpa maelekezo ya kuchukua sampuli hiyo.
Hata hivyo, Shahidi huyo alipoulizwa na Wakili wa Utetezi, Ruben Semwanzi kama anakumbuka mkojo wa Masogange una rangi gani?
Shahidi huyo alidai kuwa hajui una rangi gani maana kila mtu mkojo wake una rangi tofauti ambapo alisema>>>”Hivyo nilichukua sampuli ya mkojo wake na kuufanyia uchunguzi ambapo nilibaini una chembe chembe za dawa za kulevya Metabolite ambayo ni zao la Heroin.”
Aidha, Shahidi wa pili, ambaye ni Mpelelezi kutoka Ofisi ya ZCO, WP Judith amesema alimchukua Masogange February 15, 2017 hadi kwa Mkemia Mkuu baada ya kupewa maelekezo na Kaimu Mkuu wa Upelelezi, Ramadhan Kingai kwa lengo la kumpeleka kwa Mkemia baada ya kuambiwa Masogange anatuhumiwa kutumia na kusafirisha dawa za kulevya.
>>>”Nikiwa mapokezi kwa Mkemia nilipewa chupa ya plastic namba 446, kisha nikaelekezwa nimpeleke mshtakiwa chooni ili nichukue sampo ya mkojo wake.”
Alidai kuwa aliingia na Masogange hadi chooni na alisimama mlangoni ili kuthibitisha kama Masogange angekojoa kweli ama la na baada ya kuchukua sampuli hiyo alimkabidhi chupa Copro Sospeter ambaye alikuwa na fomu kisha wakaiwasilisha mapokezi.
Hata hivyo, shahidi huyo alipoulizwa na Wakili Semwanzi kuwa mkojo wa Masogange una rangi, alisema hakumbuki rangi akisema>>>”Sikumbuki rangi, isipokuwa inafahamika rangi ya mkojo ni ipi, ila kama ulikuwa wa rangi ya Njano Mpauko.”
No comments:
Post a Comment