Thomas Ulimwengu amefanyiwa upasuaji
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la
kulipwa katika club ya AFC Eskilstuna ya Sweden Thomas Ulimwengu
amefanyiwa upasuaji wa goti.
Thomas Ulimwengu ambaye amekuwa hafanyi vizuri wakati huu kutokana na
kusumbuliwa na goti kiasi cha kuhatarisha uwezo wake uwanjani,
amefanyiwa upasuaji tayari na kesho anaanza mazoezi ya kutembea.
Ulimwengu kupitia instagram account yake amethibitisha kufanyiwa upasuaji “Nashukuru Mungu oparation ya Goti imeenda poa na nimeshapata ruhusa tayar…kesho tunaanza mazoez ya mguu chini ya uangalizi wa doct… THANKS GOD.”
No comments:
Post a Comment