Shabiki mtoto wa soka Bradley Lowery amefariki leo
Kama ni shabiki wa soka la England najua jina la Bradley Lowery sio geni katika masikio yako kutokana na umaarufu wa mtoto aliyekuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa kupenda sana kuishabikia Sunderland.
Bradley ambaye alikuwa ana mapenzi na Sunderland amefariki leo baada
ya kusumbuliwa na kansa kwa muda mrefu, Bradley alikuwa akimpenda sana
mshambuliaji wa zamani wa Sunderland ambaye amejiunga na AFC Bournemouth
Jermain Defoe.
Shabiki huyo mtoto wa Sunderland aligundulika kuwa ana kansa akiwa na
umri wa miezi 18 lakini amefariki leo akiwa na umri wa miaka 6, taarifa
za kifo cha Bradley kimetolewa kupitia mitandao ya kijamii na wazazi
wake.
No comments:
Post a Comment