Mbunge (CHADEMA) akamatwa na Polisi Mbambabay Wilayani Nyasa.
Na Muro Tv
Mbunge Zubeda Hassan Sakuru ambaye anatoka Mkoa wa Ruvuma amekamatwa mchana huu akiwa anakamilisha maandalizi ya Kikao cha ndani Wilayani huyó.
Kikao hicho kinatarajiwa kuongozwa na Katibu Mkuu Dr Vincent Mashinji
akisaidiana na Mwenyekiti wa Kanda Mhe. Cecil Mwambe (Mb), Katibu wa
Kanda Philbert Ngatunga na Viongozi wa Mkoa wa Ruvuma na Wilaya ya
Nyasa.
Philbert Ngatunga
Katibu wa Kanda, Kusini
Katibu Mkuu wa Chama Dkt. Vincent Mashinji, Mbunge wa Jimbo la Ndanda
Cecil Mwambe ambaye pia ni Mkiti wa Chama Kanda ya Kusini pamoja na
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma Zubeda Sakuru wanashikiliwa na
Jeshi la Polisi wilayani Mbamba Bay. Wamepelekwa kituoni kuhojiwa ambapo
Katibu Mkuu Dkt. Mashinji ametakiwa kueleza kwanini yuko Mbamba Bay na
aeleze amekwenda kufanya nini.
Polisi wamemkamata Katibu Mkuu Dkt. Mashinji, Mbunge Mwambe na Mbunge Zubeda baada ya kuvamia kikao cha ndani kilichokuwa kikiendelea mjini hapo ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu Dkt. Mashinji kukagua shughuli za chama katika majimbo ya kanda hiyo iliyoanza leo.
Polisi wamemkamata Katibu Mkuu Dkt. Mashinji, Mbunge Mwambe na Mbunge Zubeda baada ya kuvamia kikao cha ndani kilichokuwa kikiendelea mjini hapo ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu Dkt. Mashinji kukagua shughuli za chama katika majimbo ya kanda hiyo iliyoanza leo.
Katibu Mkuu wa Chama Dr. Vincent Mashinji pamoja na viongozi wengine 8 wa chama wakiwemo wabunge wawili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamewekwa ndani kwa masaa 48 kwa kile ambacho OCD wa Wilaya ya Nyasa amesema ni maagizo aliyopewa.
Wanaowekwa ndani kwa masaa 48 ni;
Waliowekwa ndani ni;
1. Mhe. Dr. Vincent Mashinji (Katibu Mkuu)
2. Mhe. Cecil Mwambe (Mkiti wa Kanda na Mbunge wa Ndanda)
3. Philbert Ngatunga (Katibu wa Kanda)
4. Ireneus Ngwatura (M/kiti Mkoa)
5. Delphin Gazia (Katibu Mkoa)
6. Zubeda Sakuru (Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma)
7. AsÃa Mohamed (Afisa Kanda)
8. Cuthbert Ngwata (M/kiti Wilaya)
9. Charles Makunguru (Mwenezi Wilaya)
Awali walikuwa wamehojiwa kwa makosa ya unlawful assembly na maandamano
No comments:
Post a Comment