Header Ads

BREAKING: WAZIRI WA ELIMU KUTANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA NA UALIMU 2016/17

Tanzania
Waziri wa Elimu, Science, Teknologia na Ufundi nchini Tanzania Profesa Joyce Ndalichako
Hivi punde waziri wa elimu sayansi na teknolojia ametangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha sita uliofanyika mwezi wa tano mapema mwaka huu.

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya sekondari kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita.

Kwa ufupi
  • Jumla ya watahiniwa 75, 116, walifanya mtihani huo Mei mwaka huu.
  • Kwa upande wa watahiniwa wavulana, waliofaulu walikuwa ni 42,975 (sawa na asilimia 95.34) kati ya 46,385.
  • Taarifa iliyotolea inaonyesha kuwa watahiniwa 58,556 (asilimia 93.72) walipata daraja la kwanza hadi la tatu. Kati ya hao, wasichana ni 22, 909 na wavulana ni 35,647.

By Mwandishi Wetu, Muro Tv
Matokeo ya kidato cha sita nchini yametolewa leo Jumamosi, Julai 15, yameonyesha kuwa wasichana wameongoza kwa ufaulu ambapo kati ya wasichana 28,731 (38 asilimia) waliofanya mtihani, waliofaulu ni ni 27,577 (sawa na asilimia 97.21).
Jumla ya watahiniwa 75, 116, walifanya mtihani huo Mei mwaka huu.
Kwa upande wa watahiniwa wavulana, waliofaulu walikuwa ni 42,975 (sawa na asilimia 95.34) kati ya 46,385.
Taarifa iliyotolea inaonyesha kuwa watahiniwa 58,556 (asilimia 93.72) walipata daraja la kwanza hadi la tatu. Kati ya hao, wasichana ni 22, 909 na wavulana ni 35,647.
“Mchanganuo wa ufaulu katika madaraja unaonyesha kuwa watahiniwa walipata daraja la 1-11 umepanda kwa asilimia 0.59 kutoka asilimia 93.13 mwaka 2016 hadi 93.72 mwaka huu,” imesema taarifa hiyo na kuongeza;
Pia, ufaulu katika madaraja kwa upande wa wasichana umepanda ikilinganishwa na wavulana. Ubora wa ufaulu kwa wasichana ni asilimia 94.07 ikilinganishwa na asilimia 93.49 ya wavulana.”
Ufaulu wa masomo
Kadhalika taarifa hiyo imeonyesha kuwa ufaulu kwa watanikiwa wa shule kwa upande wa masomo, ya Sayansi, Biashara, Lugha na Sanaa, haukuonyesha tofauti kubwa ukilinganisha na mwaka jana.
Hata hivyo, ufaulu katika somo la General Studies umeshuka kwa asilimia 7.54 kutoka asilimia 71. 24 hadi 63.70.
CHANZO: Mwananchi

Chanzo cha habari hii ni www.necta.go.tz  
 

No comments:

Powered by Blogger.