Header Ads

Maamuzi ya Mahakama kwa watuhumiwa watano walioishi nchini bila kibali


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo July 25, 2017 imewahukumu wafanyakazi watano wa kampuni ya uchapaji ya CI-Group Co. Ltd kifungo cha miaka mitatu jela au faini ya Tsh. Milioni 52.5 kwa makosa mawili.
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha aliwatia hatiani wafanyakazi hao baada ya kukiri makosa mawili likiwemo la kuishi nchini isivyo halali na kuwapa adhabu ya kulipa faini ya Tsh. 500,000 kila mmoja kwa shtaka la kwanza au kifungo cha miaka mitatu jela.
Aidha, katika kosa la pili wamepewa adhabu ya kulipa faini ya Tsh. Milioni 10 kila mmoja au kifungo cha mwaka mmoja ambapo walikubali kulipa fainai.
Wafanyakazi hao ni raia watatu wa India, Shashi Upadhyay, Ashish Joshi na Mohan Gaikwad wakati watuhumiwa wengine ni raia wawili wa Pakistan ambao ni Didar Karim na Manzoor Islam.

No comments:

Powered by Blogger.