IDRIS SULTAN KUHUSU ZARI KUTOKUWA NA MAJONZI MSIBANI
Baada ya Zari ambae ni Mama watoto wa mwimbaji wa Bongofleva Diamond Platnumz
kufiwa na Mama yake mzazi na picha za msiba kusambaa, baadhi ya watu
walianza kucomment na kupost kwenye Instagram na kusema ni msiba lakini
Zari hajaonekana na sura ya majonzi.
Kila mmoja ameichukulia kwa mtazamo wake lakini Mtangazaji wa 102.5 CHOICE FM Dar es salaam na Mchekeshaji Idris Sultan ametumia time yake kuandika yafuatayo baada ya kuona watu wamezidi kumuandama Zari.
“Fanya chochote ila usiache kulia msibani, hawa Wabongo
wanahesabu hadi machozi na high tone na low tone za mlio wa Mfiwa,
utasikia pale amepanda key yupo soprano anakuja bass sasa hivi then
sauti ya 3” #SioHabari
Una maoni yoyote kuhusu hii ishu ya majonzi msibani? niachie comment yako hapa chini
No comments:
Post a Comment