Watanzania waaswa kujitokeza kuchangia damu ilikuoa Wamama Wajawazito
Watanzania wameaswa kujitokeza kuchangia
damu mara kwa mara ili kuondokana na tatizo la vifo vinavyotokana na
upungufu wa damu hasa kwa kina mama wajawazito nchini wanaopoteza damu
nyingi wakati wa kujifungua. Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati
alipotembelea katika tukio la uchangiaji damu lililofanyika Makao makuu
ya benki ya KCB jijini Dar es salaam. “Marufuku kwa mtoa huduma yeyote wa afya
kuuza damu mgonjwa kwani wananchi wanachangia damu bure kwa manufaa yao
ya baadae aidha kwa wao wenyewe au ndugu zao” alisema Waziri Ummy. Aidha Waziri Ummy amewaagiza Waganga
Wafawidhi wa mikoa kuhakikisha wanaweka mabango yanayoonyesha kuwa damu
ni bure kwa wagonjwa wote wanaohitaji huduma hiyo bila ya kubagua
mwananchi yeyote. Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa
mwananchi yeyote mwenye umri wa miaka 18, mwanamke asiye mjamzito wala
kunyonyesha na asiyekua mgonjwa kama vile kisukari,saratani na mgonjwa
wa moyo anaweza kuchangia damu. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa
benki ya KCB nchini Bw. Cosmas Kimario amesema kuwa wameamua kuaandaa
uchangiaji wa damu ili kuisadia Serikali katika sekta ya Afya hususani
katika kupunguza vifo vinavyotokana na upungufu wa damu KCB wameamua kufanya hivyo ili kuelekea
kuadhimisha siku ya kuchangia damu duniani ambayo hufanyika June 14 kila
mwaka na maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo “CHANGIA
DAMU, CHANGIA SASA CHANGIA MARA KWA MARA”.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja
na Wafanyakazi wa KCB Bank wakiwakilishwa na Mkurugenzi mtendaji wao
Cosmas Kimario (Wakwanza kushoto kwa Mh.Waziri) na wadau wa Afya wakati
alipotembelea katika tukio la uchangiaji damu lililofanyika Makao makuu
ya benki ya KCB jijini Dar es salaam.
Mfanyakazi wa KCB Bank
akijitolea damu, katika siku ya Uchangiaji damu lililofanyika katika
Makao makuu ya benki ya KCB jijini Dar es salaam.
Mfanyakazi wa KCB Bank
akijitolea damu, katika siku ya Uchangiaji damu lililofanyika katika
Makao makuu ya benki ya KCB jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na waandishi wa
habari juu ya umuhimu wa kuchangia damu kwa watu wote wakati
alipotembelea katika tukio la uchangiaji damu lililofanyika Makao makuu
ya benki ya KCB jijini Dar es salaam. FOLLOW NA LIKE PAGE YANGU YA FACEBOOK HAPA CHINI
CLICK HAPA ☛OPEN FOLLOW ACCOUNT YANGU YA INSTAGRAM
No comments:
Post a Comment