MAHAKAMA TAIWAN YAIDHINISHA NDOA YA WAPENZI WA JINSIA MOJA
DUNIANI
Mahakama Taiwan yaidhinisha ndoa ya wapenzi wa jinsia moja
Mai 25,2017 
Majaji wakuu nchini Taiwan
wameidhinisha ndoa za jinsia moja na kuifanya Taiwan kuwa nchi ya kwanza
barani Asia kuhalalisha ndoa za mapenzi ya jinsia moja.
Mahakama
kuu imesema sheria za sasa za kuwazuia watu wa mapenzi ya jinsia moja
kuoana zinakiuka haki yao ya usawa na ni kinyume cha Katiba.Mahakama hiyo imelipa bunge la nchi hiyo miaka miwili kufanyia mabadiliko ya sheria za sasa au lipitishe sheria mpya.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mahakama imesema kutowaruhusu watu wawili wa jinsia moja kuoana kwa madai ya kulinda maadili ni sawa na "ubaguzi" "bila kufuata msingi wowote"
No comments:
Post a Comment