Mbio za mwenge wa uhuru zazindua ujenzi wa kiwanja cha Philip Morris Tanzania mjini Morogoro.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kiwanda cha Philip Morris Tanzania Ltd Dagmara Piasecka
akipokea mbio za mwenge wa Uhuru baada ya kuzindua ujenzi wa kiwanda
mjini Morogoro Jumamosi .
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru AmouAmour Hamad r akikata utepe
kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi wa kiwanda cha Philip Morris
Tanzania jana mjini Morogoro. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro.
Ujenzi wa kiwanda hicho ambao utagharimu zaidi ya 60bn/- utawaongezea
faida wakulima wa zao la tumbaku hapa nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo akizungumza baada ya uwekaji
wa jiwe la msingi wa ujenzi wa kiwanda cha Philip Morris Tanzania jana
mjini Morogoro. Kulia ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad
Amour na kushoto ni mkurugenzi wa kampuni Dagmara Piasecka.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo akizungumza baada ya uwekaji
wa jiwe la msingi wa ujenzi wa kiwanda cha Philip Morris Tanzania jana
mjini Morogoro. Kulia ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad
Amour na kushoto ni mkurugenzi wa kampuni Dagmara Piasecka.
Philip Morris Tanzania yazindua ujenzi wa kiwanda Morogoro
Morogoro Jumamosi 10 Juni 2017…..Wakulima wa zao la tumbaku nchini
wanatarajia kufaika na ulimaji wa zao hilo baada ya kampuni yaPhilp
Morris Tanzania Limited kuwekeza zaid ya Sh. Bilioni 60 kwenye ujenzi wa
kiwanda kipya, eneo la Kingolwira katika Halmashauri ya Morogoro mjini.
Kampuni ya Philip Morris ambayo imekuwa ni mnunuzi mkubwa zaid wa
tumbaku inayolimwa zaidi hapa nchini ikiwa inanunua zaidi ya asilimia
40, inatarajiwa kuongeza ununuzi wake baada ya kukamilika kwa ujenzi wa
kiwanda.
Akiongea wakati wa kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho, kiongozi
wa kitaifa wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour amesema
amefurahisha na uamuzi wa kampuni ya Philip Morris Tanzania kuamua
kujenge kiwanda hapa nchini kwani mbali na kuongeza ununuzi wa zao la
tumbaku na kuongeza kipato kwa wakulima wetu, lakini pia kitatoa ajira
kwa watanzania na pia kuongeza na kukuza uchumi wa taifa. ‘Nimepata taarifa kuwa kampuni hii imekuwa ndio
inaongoza kwa kununua tumbaku ya Tanzania na sasa mmeamua kuwekeza
kwenye ujenzi wa kiwanda. Nawapongeza sana kwa kuunga mkono juhudi za
serikali ya awamu ya tano ambapo kauli mbiu yake ni Tanzania ya
viwanda.
Lakini
pia serikali imekuwa kwa muda mrefu ikitaka makampuni kuwekeza kwenye
viwada na hasa vya mazao ya kilimo kwa kunaongeza thamani ya mazao yetu
na kuongeza kipato kwa wakulima wetu,’ alisema Amour huku akiongeza kuwa
makampuni mingine yanayonunua bidhaa za mkulima ni muhimu wakawekeza
kwenye viwanda ili kupata bidhaa za mwisho zinazotengenezwa hapa nchi.
Serikali imekuwa msitari wa mbele kuunga juhudi zozote za kuinua
kipato cha wakulima wetu. Hii imejidhiirisha baada ya budget ya mwaka
kufuta baadhi ya kodi ambazo zimekuwa ni changamoto kwa wakulima. Hii
yote inaonyesha ni jinsi ngani tumekuwa msitari wa mbele kukuza sekta
hii kwa vyovyote mwekezaji yeyote inakuja na kuwekeza kwenye kilimo ni
wa kupongezwa, aliongeza Amour. Nawapa changamoto wakulima wetu wa
tumbaku kuongeza bidii ya kulima zao hilo kwani mnunuzi mkubwa wa zao
lao kwa sasa ameamua kuja na kuwekeza kwenye ujenzi wa kiwanda. Hii ni
faida kwa upande wao.
Aliongeza
Amour huku akitoa rai kwa wafanyikazi ambao watapata ajira kwenye
kiwanda hicho cha Philip Morris Tanzania kufanya kazi kwa bidii kwani
kutakuwa ni chachu ya kuvuta wawekezaji zaidi.’Uwekezaji kama huu ni
taji kwa wasomi wetu kwani kunapanua ajira hapa nchini lakini nawaomba
Watanzania ambao watapata hiyo fursa kuheshimu kanuni za ajira na kuwa
na uhusiano mwema na wawekezaji kwani kiwanda kikifanya kazi zake kwa
faida wafanyakazi pia nao watanufaika, alisema Amour.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uhusiano Philip Morris Tanzania Evans
Mlelwa amesema uamuzi wa kampuni yake kuamua kujenga kiwanda hapa
nchini kunatokana na mazingira mazuri ya biashara, amani na utulivu,
kiwango cha ukuaji wa uchumi pamoja na sera nzuri ya viwanda hapa nchini
Tanzania.
‘Manufaa ya kiwanda hiki ni katika kuongeza mapato yatokanayo na na
kodi kwa serikali, kodi ya mapato, kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na
pia kuongeza kwa ulimaji wa zao la tumbaku na kutoa ajira katika nyanja
mbali mbali kama uzalishaji na usambazaji, alisema Mlelwa huku akiongeza
kuwa kampuni yake itajikita zaidi kwenye huduma za jamii kama elimu na
kuhahakisha Wananchi wanaozunguka kiwanda wanapata maji salama kwa
matumizi ya nyumbani. ‘Wanawake wamekuwa wakisahaulika sana.
Sisi tuna mpango mzuri wa kuwawezesha na kuwainua kichumi na ndio maana
nasema kiwanda kiwanda hiki kitakapokamililika kitakuwa na manufaa mengi
kwa Wananchi wetu, alisema Mlelwa. FOLLOW NA LIKE PAGE YANGU YA FACEBOOK HAPA CHINI
CLICK HAPA ☛OPEN FOLLOW ACCOUNT YANGU YA INSTAGRAM
No comments:
Post a Comment