Walichofanya Multichoice Tanzania kwa Watoto Yatima DSM
Misaada kutoka MULTICHOICE Tanzania ilikuwepo
siku nyingi na kinachofanywa sasa ni muendelezo tu wa kilichoanzishwa
ambapo mara nyingi tumeshuhudia jinsi wanavyogusa wasiojiweza huku
mitaani kwa misaada mbalimbali.
Leo ni zamu ya Kituo cha kulelea Watoto Yatima cha Al-Madinnah kilichopo Tandale, DSM kwa kuwapa zawadi za vyakula mbalimbali kwa ajili ya Eid ikiwa ni miaka mitano sasa kwa Multchoice kutoa misaada mbalimbali kwenye kituo hicho wakitambua malezi ya watoto waishio kwenye mazingira magumu ni jukumu la kila mtu.
Meneja Operesheni wa Multichoice Baraka Shelukindo ndiye alisimamia hili zoezi mwanzo mwisho akishuhudiwa na baadhi ya mabalozi wa DStv akiwemo Hadija Kopa na Riyama Ali ambapo mbali na kukifadhi kituo hicho mara kwa mara pia walifadhili uanzishwaji wa mradi wa ushonaji.
>>> “Tunatambua
kuwa jukumu la kuwalea watoto kama hawa ambao kwa sababu moja ama
nyingine wamejikuta katika mazingira magumu ni letu sote. Hawa ni ndugu
zetu, watoto wetu, na pia ni tegemeo kubwa kwa taifa letu, hivyo
kuwasaidia ni jukumu letu.” –Shelukindo.
Al-Madinnah Orphanage Centre ni
kituo kilichoanzishwa mwaka 2004 ambapo hadi sasa kinahudumia watoto 65
ikiwa ni wavulana 40 na wasichana 25 huku wengi wao wakiwa wanafunzi wa
Shule za Msingi.
Meneja
Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Baraka Shelukindo akikabidhi
King’amuzi cha DStv kwa Mlezi wa Kituo cha Watoto Yatima Al-Madinnah
kilichopo Tandale, DSM Bi. Kuruthum Juma (wa pili kulia). Wengine ni
mabalozi maalum wa DStv Hadija Kopa (wa pili kushoto) na Riyama Ali.
Mshonaji
katika Mradi wa ushonaji wa Al-Madinnah Bi. Aziza Amri (wa pili kulia)
akiwa na Hadija Kopa (kulia), Baraka Shelukindo (wa tatu kutoka
kushoto), Kuruthum Juma (wa pili kushoto) na Riyama Ali (wa kwanza
kushoto).
Meneja
Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Baraka Shelukindo (kushoto)
akikabidhi zawadi kwa Mlezi wa kituo cha Al-Madinnah Kuruthum Juma (wa
pili kulia). Wengine Hadija Kopa na Riyama Ali.

No comments:
Post a Comment