Header Ads

Sheria 6 za ndoa zinazoshangaza, kufunga ndoa na maiti n.k

Duniani

 MuroTV

Sheria 6 za ndoa zinazoshangaza, kufunga ndoa na maiti n.k

Kwa sheria za Tanzania ndoa ni maridhiano baina ya watu wawili ambapo hutambuliwa katika Katiba ili kulinda muunganiko huo lakini zipo baadhi ya sehemu ndoa sio lazima iwe jambo la maridhiano…leo nimekutana na hizi sheria saba za ndoa kutoka sehemu mbalimbali duniani.
1: Ufaransa 
Sheria ya ndoa ya Ufaransa inaruhusu mtu kuoana na mtu aliyefariki iwapo walikubaliana kuoana kabla ya kifo ambapo kwa mujibu wa sheria hii mtu anatakiwa kuwasilisha vithibitisho kwamba marehemu alitaka kufunga ndoa na wewe. Sheria hii ilianzishwa wakati wa Vita ya Kwanza ya Dunia ambapo wanawake waliolewa na wachumba zao waliokufa kwenye vita.

2: Saudi Arabia
Mwaka 2014 Saudi Arabia ilitangaza sheria mpya ya ndoa ambapo wanaume wa nchi hiyo walikatazwa kisheria kuoa wanawake kutoka Bangladesh, Myanmar, Chad na Pakistan. Sheria hii ilianzishwa baada ya idadi kubwa ya wanaume wa Saudi kuanza kuoa wanawake kutoka mataifa hayo na kuwaacha wanawake wao bila wanaume.

3: Monaco 
Katika mji wa Monaco ni kosa kisheria kuowa/kuolewa bila kutangaza sheria hii inamlazimisha mtu kutoa tangazo maalum kwa siku kumi kabla ya harusi ambapo maharusi pia watalazimika kusubiri zipite Jumapili mbili baada ya kutangaza ndoa yao ndipo waoane.

4: Mississippi, Marekani 
Ukiwa Mississippi, Marekani ni kosa la kisheria kufunga ndoa ya kiserikali ukiwa umelewa. Sheria hii ilianzishwa ili watu waoane wakiwa na akili timamu isiyoendeshwa na pombe baada ya watu wengi kutaka kuachana baada ya kuoana wakiwa wamelewa.

5: Kansas, Marekani 
Ni kosa la kisheria kumyanyasa mama-mkwe wako ukiwa Wichita Marekani kwani sheria inawataka wanandoa kumpenda mama-mkwe ambapo mtu atakayekutwa na kosa la kumchukia mama-mkwe atakuwa na kesi ya kujibu. Sheria hii inajulikana kama “Wichita law”.

6: Hartford, Connecticut
Sheria ya Hartford, Marekani inakataza wanandoa kubusiana katika maeneo ya wazi siku za Jumapili lakini wanaruhusiwa kufanya hivyo siku nyingine. Sheria hii imewafanya wanandoa wengi kutokuoana siku za Jumapili.


MuroTV na murotv.blogspot.com zipo kwaajili ya kukuhabarisha kwa wakati.
Image may contain: text KWA MATANGAZO WASILIANA NAMI KUPITIA; 

Phone: 0768786851
Email:prospermuro690@gmail.com
          : prosperalphonce35@gmail.com
Instagram: muro_tv

 

No comments:

Powered by Blogger.