Umeshawahi ku-HACKIWA Account yako? hiki ndo kinachotekeaga
Imeandikwa na Prosper Muro
07 June, 2017 Shilole Kama wewe ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii utakuwa umekutana neno ‘Hack‘
ama kuibiwa account zamitandao ya kijamii kama ilivyomtokea mwanadada Shilole hivi karibuni kwani ameonekana akilalamika mitandaoni kuwa account yake ya Insstagram imehakiwa na mtu asie julikana. Mara nyingi watu maarufu
wamekuwa wakilalamika account zao kuwa Hacked ama kuibiwa.MxCarter ni mtaalamu wa maswala hayo na hapa ameeleza huwa inatokea vipi, chakufanya ili yasikukute na wewe. >>>Kuna njia nyingi a
ku-Hack hizi account na kwa hapa bongo wanatumia njia rahisi na mara
nyingi huwa nawaelekeza hawa mastaa maana wao ndo account zao huwa
zinafuatiliwa sana, hawa hackers wanaweza kukutumia email inayoonekana
kama Instagram ndo wamekutumia na ukibonyeza tu ile link unakuwa
umeshapatikana. >>>Ukitumiwa email
inatakiwa ujue email inasemaje kabla ya kufungua link..mtu kutoka
Instagram hawezi kukuuliza Password yako pia tusipende kuweka password
zinazohusiana na maisha yetu kama jina lako, mtoto wako, mahali
ulipozaliwa n.k.kwasababu inakuwa rahisi mtu kukisia password yako- MxCarter MuroTV na murotv.blogspot.comzipo kwaajili ya kukuhabarisha kwa wakati. KWA MATANGAZO WASILIANA NAMI KUPITIA;
No comments:
Post a Comment