Header Ads

Watu 12 wauwawa katika shambulio la kwanza la 'IS' nchini Iran

 MuroTV

Watu 12 wauwawa katika shambulio la kwanza la 'IS' nchini Iran

7 Juni 2017 
Picha hii ya kituo cha Far News inaonyeha mlipuko nje ya kaburi Picha hii ya kituo cha Far News inaonyeha mlipuko nje ya kaburi
Mashambulio mawili ya kujitoa mhanga katika Bunge la Iran na kwenye eneo la kaburi la kiongozi wa kidini Ayatollah Khomeini kwenye mji mkuu wa Iran, Tehran, yamesababisha vifo vya watu 12 na wengine wengi kujeruhiwa.
Mashambulio hayo katika jumba la Bunge, kwa sasa inaonekana imemalizika, baada ya masaa kadhaa ya kuzingirwa, huku milio ya risasi ikisikika.
Mlipuaji mmoja wa kujitoa kufa aliyekuwa amevalia vilipuzi, alijilipua katika eneo hilo la kumbukumbu na kaburi la Khomeini.
Maafisa wa usalama wa Iran wamefaulu kuzima shambulio hilo.
 Wanajeshi wa Iran wananyatia huku wakizingira majengo ya Bunge Wanajeshi wa Iran wananyatia huku wakizingira majengo ya Bunge
Mashambulio hayo yalifanyika vipi?
Watu waliokuwa wamejihami na bunduki aina ya AK, waliingia ndani ya majengo ya Bunge, Jumatano asubuhi.
Picha kutoka mahala pa tukio zilionyesha operesheni kali ya walinda usalama, huku wanajeshi wakizingira bunge.
Milio mikali ya risasi zilisikika. 
 Picha hii inaonesha mtoto akishushwa dirishani kutoka kwenye majengo ya Bunge
  Picha hii inaonesha mtoto akishushwa dirishani kutoka kwenye majengo ya Bunge 
 Kundi la Islamic State (IS), limekiri kutekeleza mashambulio hayo, ambayo ni ya kwanza kutokea nchini Iran.
IS imeweka picha mtandaoni, inayodai kuwa ni ndani ya majengo ya Bunge.
    Runinga ya taifa ya Iran baadaye iliripoti kuwa, washambuliaji wanne walioingia ndani ya majengo ya Bunge, wameuwawa na walinda usalama.
    Mamlaka kuu nchini Iran inapinga dhana kuwa, kunao watu waliozuiliwa matenga ndani ya majengo hayo ya Bunge.
    Shirika la habari la Iran IRIB lilimnukuu mbunge mmoja akisema kuwa kulikuwa na washambualiaji kadha ndani ya majengo ya bunge waliokuwa wamejihami na bunduki aina ya AK-47.
    Shirika hilo la habari lilisema kuwa walinzi wawili walijeruhiwa.
    Ripoti zinasema kuwa ufyatuaji risasi katika kaburi la Ayatollah Khomeini ulifanyika wakati mmoja.

    Shrine of the late Ayatollah Ruhollah Khomeini at Khomeini's mausoleum in Tehran (2009)
    Kaburi la Ayatollah Khomeini kusini mwa Tehran 
    MuroTV na murotv.blogspot.com zipo kwaajili ya kukuhabarisha kwa wakati.
    Image may contain: text KWA MATANGAZO WASILIANA NAMI KUPITIA; 
    Phone: 0768786851
    Email:prospermuro690@gmail.com
              : prosperalphonce35@gmail.com
    Instagram: muro_tv
     

    No comments:

    Powered by Blogger.