Header Ads

Mwanasheria Mkuu wa TBS, Baptister Marco Bitaho apandishwa kizimbani


MuroTV

Mwanasheria Mkuu wa TBS, Baptister Marco Bitaho apandishwa kizimbani


Mwanasheria Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Baptister Marco Bitaho (54) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashitaka matatu ikiwemo kuisha na kufanya kazi nchini bila kibali na kutoa taarifa za uongo ili apate hati ya kusafiria.
Bitaho ambaye ni Mkazi wa Yombo Vituka amesomewa mashitaka yake leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa wakili wa Serikali kutoka Uhamiaji, Novatus Mlay amesema, Mei 19, mwaka huu huko Kinondoni katika ofisi ya uhamiaji Bitaho akiwa raia wa Burundi alikutwa nchini Tanzania bila ya kuwa na kibali cha kumuwezesha kuishi nchini.
Aidha imedaiwa kuwa, siku na mahali hapo Mshtakiwa Bitaho alikutwa akifanya kazi kama Mwanasheria Mkuu wa TBS bila ya kuwa na kibali kinachomruhusu kufanya kazi hapa nchini.
Katika mashitaka ya tatu, Mlay amedai kuwa, Julai 6 mwaka 2011 katika ofisi ya Uhamiaji ya Dar es Salaam iliyopo wilaya ya Ilala, mshtakiwa wakiwa raia wa Burundi alitoa taarifa za uongo kuhusu maelezo yake binafsi wakati akijaza fomu ya kuomba pasi ya kusafiria namba CT (5)(Ai).
Wakili Mlay aliongeza kuwa, kitendo hicho cha kutoa taarifa za uongo kilimuwezesha Bitaho kupata pasi ya kusafiria ya Tanzania yenye namba AB 474856 huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za nchi.
MuroTV na murotv.blogspot.com zipo kwaajili ya kukuhabarisha kwa wakati.
Image may contain: text KWA MATANGAZO WASILIANA NAMI KUPITIA; 
Phone: 0768786851
Email:prospermuro690@gmail.com
          : prosperalphonce35@gmail.com
Instagram: muro_tv

No comments:

Powered by Blogger.