Header Ads

SIKU 7 ZA WABONGO KUJENGA DARAJA LA TRENI KWENYE MAJI YAENDAYO KASI

MuroTv

Siku 7 za Wabongo kujenga Daraja la Treni kwenye maji yaendayo kasi

Ni kiasi wiki moja imekatika tangu usafiri wa Treni kutoka DSM kwenda Bara usitishwe baada ya Daraja la Mto Ruvu katika Mkoa wa Pwani kusombwa na maji kutokana na mvua hivyo kuwafanya mafundi wa Rahco na TRL kufanya kazi usiku na mchana wakimuahidi Waziri wa Ujenzi kuwa wataukamilisha ujenzi huo haraka.
 zinaye Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Masanja Kadogosa  amebainisha kuwa mafundi wamefanya kazi saa 24 na kufanikiwa kufungua njia hivyo wataanza kupitisha mizigo ili kujiridhisha kabla ya kupitisha abiria.
>>>“Daraja hili lilititia, mafundi wetu wamefanya kazi usiku kucha saa 24. Napenda kuwaambia watanzania kuwa leo tunafungua njia rasmi na tutaanza kupitisha mizigo mpaka mafundi wetu watakapojiridhisha kwa mambo ya kiufundi. Tutakapoona usalama umetosha tutapitisha abiria.” – Masanja Kadogosa.

No comments:

Powered by Blogger.