RAILA ODINGA KUMFANYA MKEWE NAIBU RAIS, KENYE
MuroTv
Raila akejeliwa kumfanya mkewe Naibu Rais Kenya
Katika tamko lake lenye hisia hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii, Kuria aliwatahadharisha wanasiasa Kalonzo Musyoka na Musalia Mudavad kuwa makini dhidi ya Raila.
Asema Raila akipata madaraka ya kuwa Rais wa Kenya, atawajaza ndugu zake katika nafasi alizowaahidi wenzake katika vyama vya umoja huo siku moja baada ya Raila kuwasilisha nyaraka zake kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwa ajili ya uhakiki hivi karibuni.
Mbunge huyo wa Gatundu Kusini alimwelezea Raila kama mtu mwenye tatizo kubwa kama vile anataka kunywa sumu huku akitaraji Rais Uhuru Kenyatta afariki dunia. Siku chache zilizopita Tume Huru ya Uchaguzi Kenya (IEBC) imewaidhinisha wanasiasa wanane watakaowania urais katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti, mwaka huu.
Walioidhinishwa ni pamoja na Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee atakayewania kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa pili, na kiongozi wa muda mrefu wa upinzani Raila Odinga anayewania urais kwa mara ya nne. Raila aliyehudumu kama Waziri Mkuu katika Serikali ya Muungano ya Rais Mwai Kibaki kati ya 2008 na 2013, anawania urais chini ya umoja wa vyama vya upinzani unaojulikana kwa jina la Nasa.
Katika Uchaguzi Mkuu ujao nchini Kenya Agosti 8, mwaka huu, ushindani mkubwa unatarajiwa kuwa kati ya Kenyatta na Raila huku ukirejesha nchi hiyo katika historia ya siasa kati ya baba wa wagombea hao.
Rais wa Kwanza wa Kenya Jommo Kenyatta ndiye baba wa Rais Uhuru Kenyatta huku Jaramogi Odinga Oginga aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais baada ya uhuru wa nchi hiyo mwaka 1963, akiwa baba wa Odinga.
No comments:
Post a Comment