NAVY KENZO KUHUSU WIMBO WA BEN POL NA PICHA ZAKE ZA UTATA
Mix
Navy Kenzo kuhusu wimbo wa Ben Pol na picha zake za utata
Aika na Nahrel wamefunguka kupitia XXL ya Clouds FM leo June 2, 2017 wakisema wimbo mpya wa Ben Pol unaoitwa Tatu ni mbaya na hauendani na namna alivyopiga picha na kupakwa mafuta:>>>“Unajua Tanzania tuna utamaduni wetu. Nadhani hata Baraka maoni yake siyo kashfa lakini ni maoni yake. Tuna utamaduni binafsi tunachukulia vitu kibinadamu lakini nadhani maoni yanaruhusiwa.” – Nahrel.
“Ulichokisema na sisi tulikiongea vivyo hivyo. Nahrel baada ya kuona Baraka the Prince ametuma ile comment kwenye Group tulisema kwamba wasanii wote kama wangekuwa na uwezo kama wa Baraka the Prince kuongea kile wanachojisikia moyoni, basi nafikiria tungeenda mbali sana maana wengi sana wanakuwa wandanganyana (Siyo mimi lakini nimesema kuwa nyimbo mbaya)”. – Aika.

No comments:
Post a Comment