Mwimbaji Tekno amekuandikia maneno 60 ya Kiswahili kuhusu ngoma yake
MuroTV
Burudani
Mwimbaji Tekno amekuandikia maneno 60 ya Kiswahili kuhusu ngoma yake
Lugha
ya Kiswahili inazidi kuzichukua headlines duniani kutokana na kutumiwa
na mastaa wakubwa kila siku, leo nimeipata hii ya staa mwimbaji
wa Nigeria, Tekno ambaye ameachia single yake mpya na ameamua kuitangaza
kwa lugha ya Kiswahili kuwa inapatikana kwenye wasafi.com.
Tekno ameandika
>>>”Wanasema Utamu wa Ngoma uingie Ucheze….Haya watoto wazuri
na wanangu wote wa Bongo Land ardhi ya Nyerere, twendeni tukaonje Huu
Utamu Wa Pini yangu mpya ya kuitwa #SAMANTHA ila sio Mbwana”<<<…..
“Ngoma iko Ndani Ya @wasafidotcom Kwa Mtonyo Wa Tsh 300 tu, Alafu Uje Unambie Umeionaje….Naskia eti Ngoma za Tekno hazijawai kumuacha mtu Salama…..Haya twendeni tukaliamshe Dudeeeee!!! – Tekno
MuroTV na murotv.blogspot.com zipo kwaajili ya kukuhabarisha kwa wakati.
KWA MATANGAZO WASILIANA NAMI KUPITIA;

No comments:
Post a Comment