Mtu mmoja afariki katika shambulio eneo la Daraja la London
MuroTv
London
Mtu mmoja afariki katika shambulio eneo la Daraja la London
4 June, 2017
Mtu mmoja amefariki
dunia na wengine kadha kujeruhiwa katika tukio lililohusisha watu
kugongwa na gari na wengine kuchomwa visu katika eneo la Daraja la
London.
Polisi wa Uchukuzi Uingereza wanasema walipokea taarifa za watu kugongwa kwa gari katika daraja hilo.Maafisa wenye silaha walitumwa eneo hilo baada ya watu walioshuhudia kusema gari la rangi jeupe lilivurumishwa kutoka kwenye barabara na kuwagonga watu waliokuwa wakipita.
Maafisa walitumwa pia katika Soko la Borough, ambapo inadaiwa watu walishambuliwa na kuchomwa visu.
Daraja la London kwa sasa limefungwa.
Mabasi yanaelekezwa kwingine. Daraja la Southwark lililoko karibu pia limefungwa.
Shirika la Uchukuzi London (TfL) limesema babarara ya Borough High pia imefungwa, na taarifa zinasema maafisa wa polisi wenye silaha wameonekana maeneo hayo.
KWA MATANGAZO WASILIANA NAMI KUPITIA;
Phone: 0768786851
Email:prospermuro690@gmail.com
: prosperalphonce35@gmail.com
Instagram: muro_tv
No comments:
Post a Comment