BREAKING: Watu kadha wagongwa na Gari Daraja la London
MuroTv
London
Watu kadha wagongwa na Gari Daraja la London
4 June, 2017
Taarifa zinasema
watu kadha wamejeruhiwa katika tukio lililohusisha watu kugongwa na gari
na wengine kuchomwa visu katika eneo la Daraja la London.
Polisi wa Uchukuzi Uingereza wanasema walipokea taarifa za watu kugongwa kwa gari katika daraja hilo.Maafisa wenye silaha walitumwa eneo hilo baada ya watu walioshuhudia kusema gari la rangi jeupe lilivurumishwa kutoka kwenye barabara na kuwagonga watu waliokuwa wakipita.
Maafisa walitumwa pia katika Soko la Borough, ambapo inadaiwa watu walishambuliwa na kuchomwa visu.
Daraja la London kwa sasa limefungwa.
Mabasi yanaelekezwa kwingine. Daraja la Southwark lililoko karibu pia limefungwa.
Shirika la Uchukuzi London (TfL) limesema babarara ya Borough High pia imefungwa, na taarifa zinasema maafisa wa polisi wenye silaha wameonekana maeneo hayo
Maafisa wa polisi wenye silaha wametumwa barabara ya Borough High
Polisi na magari ya kubebea wagonjwa katika upande wa kusini wa Daraja la London
Rangi za taa za magari ya maafisa wa huduma za dharura zikioneakna eneo la Daraja la Londongari lililohusika lilikuwa linaendeshwa na mwanamume na lilikuwa linaenda kwa kasi ya karibu maili 50 kwa saa.
Watu hao watano au sita wanatibiwa, amesema.
Bi Jones anasema gari hilo lilikuwa linasafiri kutoka katikati mwa London na lilielekea upande wa kusini wa mto.
Anasema baadaye aliona mwanamume akikamatwa na kutiwa pindi na maafisa wa polisi.
Bi Jones anasema mwanamke Mfaransa ni miongoni mwa waliojeruhiwa.
Twitter
Maafisa wa Magari ya kuwabeba wagonjwa wa London, moja ya idara za kwanza kuzungumzia tukio hilo, walisema wanashughulikia kisakikubwa eneo la Daraja la London na kuwatahadharisha watu wasielekee eneo hilo.
KWA MATANGAZO WASILIANA NAMI KUPITIA; Phone: 0768786851
Email:prospermuro690@gmail.com
: prosperalphonce35@gmail.com
Instagram: muro_tv


No comments:
Post a Comment