Maneno ya Babu Tale kwa DJ Choka baada ya kuweka wazi kuwa aliugua TB
Meneja wa kundi la Tip Top Connection pamoja na mwimbaji staa wa Bongofleva Diamond Platnumz, Babu Tale ameizungumzia issue ya DJ Choka kuweka wazi kuwahi kuugua ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) mpaka alivyopata matibabu na kupona.
Babu Tale alitumia ukurasa wake wa Instagram kumpongeza DJ Choka
kwa kuamua kuweka wazi alichokuwa anaumwa akisema ni mfano wa kuigwa
kwani watu wengi wamekuwa wanaficha juu ya magonjwa yanayowakibili.
“Wahenga walisema mficha uchi hazai, wakazidi kusema
mficha maradhi kifo humuumbua, kwanza kabisa nimeguswa na kufurahishwa
na kitendo cha kijasiri alicho kifanya ndugu yangu @chokadj kwa kuiwekea wazi jamii nini alikwa anaumwa na kwa kudra zake Mungu akapona.
“Imekuwa ni jadi sikuhizi
kwa vijana wengi alwatan kuficha maradhi yao huku wakisahau hofu na
wasiwasi pia nayo ni ugonjwa, na kadri unavo zidi kuficha ndivyo kadri
ugonjwa unazidi kukomaa.
“@chokadj
kawa mfano mzuri kwa jamii yetu ya sasa kudhihirisha kuwa kuficha
maradhi si suluhisho wa tiba ya ugonjwa wako, ni wangapi jana walikuwa
wamejifungia ndani wakiugulia TB huku mioyo yao ikiamini TB haitibiki
lakini baada ya @chokadj
kujitokeza na kuiambia jamii ameuguwa ugonjwa huo na kupona leo
wagonjwa hao hao wapo kwenye foleni hospitalini wakingojea huduma ya
matibabu.
Ndugu zangu halimpati mtu
jambo isipo kuwa Mungu kutaka kwan kwa hakika ni yeye pekee atupae
mitihani na majibu yake akakupatia. Sasa nazidi kuaminu TB ina tibika. #AsanteChoka“ – Babu Tale.
No comments:
Post a Comment