HAKUNA SHERIA INAYORUHUSU ASKARI POLISI KUVUNJA SHERIA
‘Hakuna sheria inayoruhusu askari Polisi kuvunja sheria’
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi amesema
kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hakuna sheria
yoyote inayowapa haki wanajeshi kuwatesa raia au kuvunja sheria.
Dk Mwinyi alitoa ufafanuzi wa mfumo huo wa jeshi wakati akijibu swali
la Mbunge wa Viti Maalum, Lucy Magereli (Chadema) aliyetaka kujua ni
sheria zipi zinawapa askari haki ya kutesa raia.
Alisema matukio ya wanajeshi kushambulia raia au raia kushambulia
wanajeshi, mara nyingi yamekuwa yakijitokeza wakati pande mbili
zimetofautiana kauli, katika ulevi, wivu wa kimapenzi na hata ujambazi.
Dk Mwinyi alisema, katika kushughulikia hali hiyo, mara nyingi kesi
hufunguliwa kwenye mahakama za kiraia na hukumu hutolewa kwa mujibu wa
sheria zilizopo nchini. “Hakuna mtu aliye juu ya sheria na inashauriwa
kwamba watu wanaokumbwa na kadhia ya kushambuliwa na askari wapeleke
mashtaka kwa mujibu wa taratibu zilizipo ili sheria ifute mkondo wake.”
“Kwa taratibu za Jeshi la Ulinzi, afisa au askari anapotiwa hatiani
na mahakama za kiraia na kuhukumiwa adhabu ya kifungo au nyinginezo,
hupoteza sifa za kuendelea kulitumikia JWTZ,” alisema. Mwinyi alisema,
maafisa na askari wa jeshi wamekuwa wakiaswa kuishi kwa kuzingatia
sheria, kanuni na taratibu zilizipo nchini.
No comments:
Post a Comment