Header Ads

Hekaheka iliyotokea mbele ya Makamu wa Rais leo June 16, 2017

MuroTV

HekaHeka

Hekaheka iliyotokea mbele ya Makamu wa Rais leo June 16, 2017

Hekaheka leo June 16, 2017 imetokea Viwanja vya Shule ya Msingi Kinyerezi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Wilaya ya Ilala ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Wakati shughuli hizo zikiendelea ghafla alitokea mtoto mdogo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka mitatu ambaye alianza kulia na kugaragara chini kitendo kilichopelekea MC kutangaza ili kujua ni mtoto wa nani.
Kutokana na kitendo cha mtoto huyo kugaragara chini kilimsikitisha Makamu wa Rais ambaye aliagiza mtoto huyo apelekwe Ustawi wa Jamii na huyo mzazi wake akamchukulie huko ambapo baada ya maamuzi hayo watu walishangalia kabla ya mzazi wa mtoto huyo kujitokeza kuomba msaada wa kusikilizwa lakini mtoto alishatolewa.

No comments:

Powered by Blogger.