Habari njema kutoka Afrika Kusini baada ya Taifa Stars kutoka sare vs Mauritius
Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambayo ipo kwenye
michuano ya COSAFA 2017 inayoendelea Afrika Kusini, leo June 29, 2017
ilirudi uwanjani kucheza mchezo wa mwisho Kundi A dhidi ya Mauritius
huku Malawi wakicheza dhidi ya Angola.
Katika Kundi A timu zote nne zilikuwa na nafasi ya kufuzu hatua
inayofuata kabla ya michezo ya leo ambapo Tanzania na Angola zikihitaji
ushindi au sare ya magoli ili mmoja kati yao afuzu, Malawi na Mautius
kila mmoja alikuwa anahitaji ushindi.
Taifa Stars imefanikiwa kufuzu hatua ya robo-fainali ya COSAFA 2017
baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Mauritius ikiwa ni dakika moja baada ya
Mauritius kupata goli la kuongoza dakika ya 67, Simon Msuva
aliisawazishia Taifa Stars dakika ya 68.
Mchezo wa Malawi na Angola nao ulimalizika kwa sare ya 0-0 na
kutokana na matokeo hayo Tanzania imesonga mbele na itacheza na Afrika
Kusini baada ya kuongoza kwa tofauti ya magoli licha ya kuwa na point 5
sawa na Angola. Malawi na Mautius zimemaliza zikiwa na point 2 kila moja
katika hatua hiyo ya makundi.
No comments:
Post a Comment