Habari kubwa mbili zilizoripotiwa kwenye Taarifa ya Habari usiku wa jana
Usiku wa June 29, 2017 zimeripotiwa taarifa mbalimbali kwenye Televisheni za Tanzania ambapo kama ulikosa hii ni time yako kuzisoma hizi kupitia murotv.blogspot.com ambapo miongoni mwa habari nyingi hizi hapa ni kubwa mbili zilizosomwa Channel 10 na TBC1
Habari ya Channel 10 – Mahakama yawakubali mawakili wapya 248
Mahakama Kuu ya Tanzania imewakubali Mawakili 248
ambao watakwenda kufanya kazi katika Mahakama mbalimbali nchini kwa
lengo la kuwawezesha wananchi kupata msaada wa kisheria na kuepuka
rushwa.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma
amesema kuongezeka kwa idadi ya Mawakili kutasaidia nchi kufikia
malengo yake ikiwemo kutafsiri mikataba mbalimbali na kuwafikishia
msaada wa kisheria wananchi walio pembezoni.
>>>“Huo
weledi waendele kuwa nao iliwaweze kuwatumikia wananchi, jambo linguine
ni swala la madili na rushwa ni swala lisilo la kufumbiwa macho
linaongelewa.” Prof. Ibrahim Juma.
“Kwa idadi ya walioingia leo
248, kutakuwa na Mawakili 6,329 ambao ni Mawakili binafsi. Kwa hiyo,
kuna uwezokano mkubwa wa kuongezeka kwa huduma za kiwakili na huduma za
kisheria kutokana na kuongezeka kwa idadi ya Mawakili. Ni jambo jema” – Tundu Lissu (Rais wa Chama cha Wanasheria).
Habari ya TBC1 – Serikali kuhusu mtandao wa Dawa za Kulevya
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
amesema Serikali imedhamiria kuendelea kupambana kutokomeza na kuvunja
mitandao ya waingizaji, wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya nchini.
Akizungumza kwenye Maadhimisho ya Dawa
za Kulevya yaliyofanyika kitaifa Dodoma, Waziri Mkuu Majaliwa amewataka
Wananchi kuendelea kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na dawa hizo.
>>>“Kila
Mtanzania aumie kwa hili na kila mmoja apate uchungu kwa hili kwamba ni
jambo lisilokubalika ndani nchi yetu na kwa maana hiyo lazima tuape
mbele yenu tutapambana na kila mmoja anayetumia, anayesambaza, anayekula
dawa za kulevya na wala usifanye mzaha na usijaribu.” – Kassim Majaliwa.
No comments:
Post a Comment