Boko Haram washambulia tena Nigeria
MuroTV
Boko Haram washambulia tena Nigeria
7 June 2017
Wapiganaji wa Boko Haram
Wapiganaji wa Boko Haram wamefanya mashambilizi makali katika mji ulioko kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Watu
walioshuhudia wanasema mashambulizi hayo makali yametokea wakati
waislamu wakijiandaa kufuturu katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa
Ramadhan.Picha ya video ambayo haijathibitishwa iliyotumwa katika mtandao wa Twitter inaonesha wanawake na watoto wakikimbia kutokana na mashambulizi hayo.
Gavana wa mji huo Kashim Shettima amesema kwamba kulikuwa na majeruhi.
Lakini hata hivyo amesema jeshi la nchi hiyo limejibu mashambulizi na mji tayari ni shwari.
Wapiganaji wa Boko Haram wameteketeza eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria kwa kuua maelfu ya watu na kulazimisha wengine milioni mbili kuyakimbia makazi yao.
MuroTV na murotv.blogspot.com zipo kwaajili ya kukuhabarisha kwa wakati.
KWA MATANGAZO WASILIANA NAMI KUPITIA;

No comments:
Post a Comment